-
“Badala ya Dhahabu, Nilipata Almasi”Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
-
-
Upesi Michael Triantafilopoulos aliyenibatiza katika kiangazi cha 1935—zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuwa nimeanza huduma ya wakati wote, alijiunga nami! Usafiri wa umma haukupatikana, kwa hiyo tulitembea kwenda kila mahali. Tatizo letu kubwa lilikuwa upinzani wa makasisi, ambao wangefanya chochote kutuzuia. Likiwa tokeo, tulikabili ubaguzi mwingi. Hata hivyo, vijapokuwa vizuizi, ushahidi ulitolewa, na jina la Yehova likatangazwa kotekote.
-
-
“Badala ya Dhahabu, Nilipata Almasi”Mnara wa Mlinzi—1997 | Machi 1
-
-
Siku moja Ndugu Triantafilopoulos nami tulikuwa tukihubiri katika kijiji cha Mouríki katika wilaya ya Boeotia. Tuligawanya kijiji katika sehemu mbili, nami nikaanza kuhubiri katika miteremko iliyo wima, kwa kuwa nilikuwa mchanga zaidi. Kwa ghafula nikasikia mayowe kutoka chini. Nilipokuwa nikikimbia kuelekea chini, nilifikiri ‘Ndugu Triantafilopoulos anapigwa.’ Wanakijiji walikuwa wamekusanyika katika mkahawa wa huko, na kasisi mmoja alikuwa akitembea kwa kishindo kwenda na kurudi kama fahali mwenye hasira. “Watu hawa hutuita ‘mbegu ya Nyoka,’” alikuwa akipiga kelele.
Huyo kasisi alikuwa tayari amevunja bakora kichwani pa Ndugu Triantafilopoulos, na damu ilikuwa ikitiririka usoni pake. Baada ya kusafisha hiyo damu, tuliweza kuondoka. Tulitembea kwa muda wa saa tatu hadi tukafika jiji la Thebes. Huko, lile jeraha lilitibiwa katika kliniki. Tuliripoti hicho kisa kwa polisi, na mashtaka yakapelekwa mahakamani. Hata hivyo, huyo kasisi alikuwa na mahusiano na wenye mamlaka, naye akaachiliwa hatimaye.
Tulipokuwa tukihubiri mji wa Leukas, wafuasi wa mmoja wa viongozi wa kisiasa wa hilo eneo “alitukamata” na kutuleta kwenye mkahawa wa kijiji, ambako tulishtakiwa katika mahakama isiyo halali. Huyo kiongozi wa siasa pamoja na wanaume wake walituzunguka-zunguka kwa zamu wakitutolea hotuba—wakifuliza kutoa maneno yenye ukali—na kututisha kwa ngumi zilizokunjwa. Wote walikuwa wamelewa. Mashutumu yao dhidi yetu yaliendelea kutoka adhuhuri hadi machweo, lakini tulibaki watulivu na kuendelea kutabasamu huku tukitangaza kutokuwa kwetu na hatia na kusali kimya-kimya kwa Yehova Mungu ili kupata msaada.
Wakati wa jioni-jioni polisi wawili walituokoa. Walitupeleka kwenye kituo cha polisi, wakatutendea vyema. Ili kutetea vitendo vyake, huyo kiongozi wa kisiasa alikuja siku iliyofuata na kutushtaki juu ya kueneza propaganda dhidi ya Mfalme wa Ugiriki. Kwa hiyo polisi walitupeleka, huku tukisindikizwa na wanaume wawili, hadi mji wa Lamia kwa uchunguzi zaidi. Tuliwekwa kizuizini kwa siku saba kisha tukapelekwa tukiwa tumetiwa pingu mikono hadi mji wa Larissa ili kuhukumiwa.
Ndugu zetu Wakristo katika Larissa, waliokuwa wamejulishwa mapema, walingojea kufika kwetu. Shauku kuu waliyotuonyesha ilikuwa ushahidi mzuri kwa walinzi. Wakili wetu, mmoja wa Mashahidi wa Yehova aliyekuwa kanali luteni hapo zamani, alijulikana sana mjini. Alipokwenda mbele mahakamani na kutoa hoja juu ya kesi yetu, yale mashtaka dhidi yetu yalifunuliwa kuwa yasiyo ya kweli, nasi tukaachiliwa.
Mafanikio ya ujumla ya mahubiri ya Mashahidi wa Yehova yaliongoza kwenye kuongezeka kwa upinzani. Sheria zilipitishwa katika mwaka wa 1938 na wa 1939 zilizokataza ugeuzaji wa imani, na Michael nami tulihusika katika kesi nyingi za mahakama juu ya suala hilo. Baadaye, ofisi ya tawi ilitushauri kutohubiri pamoja ili tusivute uangalifu mwingi kwenye utendaji wetu.
-