-
Nilipata Majaribu Makali SanaMnara wa Mlinzi—2003 | Februari 1
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 27]
Makrónisos ni Kisiwa cha Kutisha
Kwa muda wa miaka kumi, kuanzia 1947 hadi 1957, wafungwa 100,000 walipelekwa kwenye kisiwa kame cha Makrónisos. Miongoni mwao walikuwa Mashahidi waaminifu wengi sana waliopelekwa huko kwa sababu ya msimamo wao wa Kikristo wa kutounga mkono upande wowote katika vita. Mara nyingi wale waliochochea wahamishwe walikuwa makasisi wa Kanisa Othodoksi la Ugiriki ambao waliwashtaki Mashahidi kwa uwongo kuwa Wakomunisti.
Kuhusu mbinu za eti “kuwarekebisha wakosaji” zilizotumiwa huko Makrónisos, kitabu cha marejezo cha Kigiriki kinachoitwa Papyros Larousse Britannica kinasema hivi: “Mbinu katili za mateso, . . . hali ya makao, ambayo haipaswi kuonekana katika nchi iliyostaarabika, na jinsi walinzi walivyowavunjia wafungwa heshima . . . hayo yote ni aibu kubwa kwa nchi ya Ugiriki.”
Baadhi ya Mashahidi waliambiwa kwamba hawangeachiliwa kamwe kama hawangekana imani yao. Hata hivyo, Mashahidi walikuwa waaminifu. Isitoshe, baadhi ya wafungwa wa kisiasa walikuja kukubali kweli ya Biblia kwa sababu walifungwa pamoja na Mashahidi.
[Picha katika ukurasa wa 27]
Minos Kokkinakis (wa tatu kutoka kulia) na mimi (wa nne kutoka kushoto), tukiwa kwenye kisiwa cha Makrónisos
-
-
Nilipata Majaribu Makali SanaMnara wa Mlinzi—2003 | Februari 1
-
-
Tuliambiwa kwamba tungepelekwa hadi Makrónisos, kisiwa kame karibu na pwani ya Athens, Ugiriki. Hata kusikia jina Makrónisos kulifanya watu waogope kwa kuwa wafungwa waliokuwa katika gereza hilo waliteswa na walilazimishwa kufanya kazi ngumu sana. Tulipitia Piraeus tulipokuwa njiani kwenda huko. Ijapokuwa tulikuwa tumefungwa pingu, tulitiwa moyo wakati baadhi ya waamini wenzetu walipoingia melini na kutukumbatia.—Matendo 28:14, 15.
Maisha huko Makrónisos yalikuwa yenye kutisha. Wanajeshi waliwatesa wafungwa tangu asubuhi mpaka usiku. Wafungwa wengi wasiokuwa Mashahidi walirukwa na akili, wengine wakafa, na wengi wakatoka wakiwa walemavu. Usiku tulisikia kilio cha wale waliokuwa wakiteswa. Blanketi yangu nyembamba haikunikinga na baridi usiku.
Muda si muda, Mashahidi wa Yehova walikuja kujulikana kambini kwa kuwa jina hilo lilitajwa kila asubuhi wafungwa walipoitwa majina kulingana na orodha. Kwa hiyo, tulikuwa na fursa nyingi za kutoa ushuhuda. Hata nilikuwa na pendeleo la kubatiza mfungwa mmoja wa kisiasa aliyekuwa amefanya maendeleo na kujiweka wakfu kwa Yehova.
Nilipokuwa uhamishoni niliendelea kumwandikia mke wangu mpendwa, lakini yeye hakuniandikia hata barua moja. Hata hivyo, niliendelea kumwandikia kwa upendo ili kumfariji na kumhakikishia kwamba hali hiyo ilikuwa ya muda tu na hatimaye tungeishi kwa furaha tena.
Idadi ya Mashahidi iliongezeka ndugu wengine walipowasili. Kwa kuwa nilifanya kazi ofisini, nilianzisha urafiki na kanali msimamizi wa kambi hiyo. Alistahi Mashahidi, kwa hiyo sikuogopa kumwomba aruhusu tutumiwe vichapo vya Biblia kutoka katika ofisi yetu huko Athens. “Jambo hilo haliwezekani,” akasema, “lakini watu wenu huko Athens wanaweza kuvifunga, kuandika jina langu juu yake, na kuvituma kwangu.” Nilipigwa na butwaa! Siku chache baadaye tulipokuwa tukiteremsha mizigo kutoka katika meli iliyokuwa imeingia, polisi mmoja alimsalimu kanali na kumwambia hivi: “Bwana, mzigo wako umefika.” “Mzigo upi?” akauliza. Kwa kuwa nilikuwa karibu na nikasikia mazungumzo hayo nikamnong’onezea hivi: “Yaonekana huo ni ule mzigo wetu ambao ulitumwa kwa jina lako kama ulivyosema.” Hiyo ilikuwa njia moja ambayo Yehova alitumia kutulisha kiroho.
Baraka Isiyotarajiwa, Kisha Mateso Mengine
Mwishoni mwa mwaka 1950 niliachiliwa. Nilirudi nyumbani nikiwa mgonjwa na nimekonda sana, na sikujua kama ningekaribishwa. Nilifurahi sana kumwona mke wangu na watoto wangu tena!
-