-
Kufanya Kazi Katika “Shamba” Kabla ya MavunoMnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
-
-
Nuru Yaangaza Zaidi
Miongoni mwa watu hao mwanzoni mwa karne ya 19, kulikuwako Henry Grew (1781-1862), kutoka Birmingham, Uingereza. Alipokuwa na umri wa miaka 13, alisafiri kwa meli pamoja na familia yake kuvuka Atlantiki na kuwasili Marekani Julai 8, 1795. Wakaanza kuishi Providence, Rhode Island. Wazazi wake walimfundisha hatua kwa hatua kuipenda Biblia. Akiwa na umri wa miaka 25 mwaka wa 1807, Grew alialikwa atumikie akiwa pasta wa Kanisa la Baptisti, katika Hartford, Connecticut.
Alichukua madaraka yake ya kufundisha kwa uzito na kujaribu kusaidia wale waliokuwa chini ya utunzaji wake waishi kupatana na Maandiko. Hata hivyo, aliamini kwamba lazima kutaniko libaki safi bila kuchafuliwa na mtu yeyote aliyezoea dhambi kimakusudi. Nyakati fulani, yeye pamoja na watu wengine wenye madaraka katika kanisa, walilazimika kuwafukuza (kuwatenga na ushirika) wale waliofanya uasherati au waliokuwa na mazoea machafu.
Kulikuwa na matatizo mengine kanisani yaliyomsumbua. Walikuwa na watu walioshughulikia mambo ya kifedha ya kanisa na kuongoza nyimbo kwenye ibada ilhali hawakuwa washiriki wa kanisa. Watu hao wangeweza kutoa maoni kuhusu mambo mazito ya kutaniko na hivyo kudhibiti mambo ya kanisa kwa kiasi fulani. Akitegemea kanuni ya kujitenga na ulimwengu, Grew aliamini kwa dhati kwamba ni wanaume waaminifu peke yao wanaopaswa kufanya kazi hizo. (2 Wakorintho 6:14-18; Yakobo 1:27) Kulingana na maoni yake, kuruhusu wasioamini waimbe nyimbo za kumsifu Mungu ni kukufuru. Kwa sababu ya msimamo huo, Henry Grew alikataliwa na kanisa mwaka wa 1811. Washiriki wengine waliokuwa na maoni kama yake walijitenga na kanisa wakati huohuo.
Kujitenga na Jumuiya ya Wakristo
Washiriki wa kikundi hiki, kutia ndani Henry Grew walianza kujifunza Biblia wakiwa na lengo la kupatanisha maisha na matendo yao na shauri la Biblia. Baada ya muda mfupi, funzo lao liliwapa uelewevu zaidi wa Biblia na wakaanza kufunua makosa ya Jumuiya ya Wakristo. Kwa mfano, mwaka wa 1824, Grew aliandika hati yenye sababu nzuri ya kukanusha Utatu. Ona jinsi kifungu hiki kutoka kwa maandishi yake kinavyopatana na akili: “‘Habari ya siku ile, na saa ile hakuna [mtu] aijuaye, wala malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila BABA.’ [Marko 13:32] Ona hapa tofauti iliyopo kati ya vyeo vya watu hao. Mwanadamu, Malaika, Mwana, Baba. . . . Bwana wetu anatufundisha kwamba ni Baba pekee aliyejua siku hiyo. Lakini hiyo si kweli, ikiwa, kama wengine wanavyodhani, Baba, Neno, na Roho Takatifu ni watu watatu katika Mungu mmoja; kwa kuwa kulingana na hili [fundisho la Utatu,] . . . Mwana aliijua kama vile Baba.”
Grew alifunua unafiki wa makasisi na makamanda wa kijeshi waliojidai kuwa wanamtumikia Kristo. Mwaka wa 1828 alitangaza hivi: “Je, twaweza kuona jambo baya kushinda kumwona Mkristo akitoka katika chumba chake cha faragha, alipokuwa akiwaombea maadui wake, na baada ya hapo kuamrisha jeshi lake litumie silaha kwa ukatili kuua maadui haohao? Kwa upande mmoja, inafurahisha kwamba anafanana na Bwana wake anayekufa; lakini anafanana na nani kwa upande mwingine? Yesu aliwaombea wale waliomwua. Wakristo huwaombea watu na kuua watu haohao.”
Grew aliandika hivi kwa mkazo hata zaidi: “Ni lini tutakapomwamini Mweza Yote anayetuhakikishia kwamba ‘hadhihakiwi?’ Ni lini tutakapoelewa asili, mtazamo, wa ile dini takatifu inayotaka tujiepushe hata na ‘kuonekana tu kwa uovu?’ . . . Je, huko si kumkashifu Mwana wa Mungu, kudhani kwamba dini yake hutaka mtu atende kama malaika kwa upande mmoja, na kumruhusu atende kama roho mwovu kwa upande mwingine?”
Uhai wa Milele Si Jambo la Asili
Katika miaka hiyo wakati ambapo hakukuwa na redio na televisheni, njia mashuhuri ya kueleza maoni ilikuwa kuandika na kugawanya vijitabu. Yapata mwaka wa 1835, Grew aliandika kijitabu cha maana kilichofunua kwamba mafundisho ya kutokufa kwa nafsi na moto wa mateso si ya Kimaandiko. Alihisi kwamba mafundisho hayo yalimkufuru Mungu.
Kijitabu hicho kingekuwa na matokeo makubwa sana. Mwaka wa 1837, George Storrs mwenye umri wa miaka 40 alipata nakala moja kwenye garimoshi. Storrs alikuwa mzaliwa wa Lebanon, New Hampshire, lakini wakati huo alikuwa anaishi Utica, New York.
Alikuwa mhudumu mashuhuri sana katika Kanisa la Methodisti-Episkopali. Aliposoma kijitabu hicho, alivutiwa kuona jinsi hoja nzuri zilivyotolewa kupinga mafundisho ya msingi ya Jumuiya ya Wakristo, ambayo hakuwa amepata kuyatilia shaka. Hakujua mwandishi wa kijitabu hicho, na alikuja kukutana tu na Henry Grew miaka kadhaa baadaye, mwaka wa 1844, wakati ambapo wote wawili walikuwa wanaishi Philadelphia, Pennsylvania.
-
-
Kufanya Kazi Katika “Shamba” Kabla ya MavunoMnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
-
-
Storrs na Grew walifanya mijadala pamoja kupinga fundisho la kutokufa kwa nafsi. Grew aliendelea kuhubiri kwa bidii hadi alipokufa Agosti 8, 1862, huko Philadelphia.
-
-
Kufanya Kazi Katika “Shamba” Kabla ya MavunoMnara wa Mlinzi—2000 | Oktoba 15
-
-
Kwa mfano, Grew, alielewa kwamba fidia ilitolewa na Yesu, lakini hakuelewa kwamba ilikuwa “fidia inayolingana,” yaani, uhai mkamilifu wa kibinadamu wa Yesu uliotolewa badala ya uhai mkamilifu wa kibinadamu uliopotezwa na Adamu. (1 Timotheo 2:6) Pia Henry Grew aliamini kwa makosa kwamba Yesu angerudi na kutawala duniani kwa kuonekana. Hata hivyo, Grew alihangaikia kutakaswa kwa jina la Yehova, jambo ambalo halikuwapendeza watu wengi tangu karne ya pili W.K.
-