Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kukabiliana na Huzuni
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 1
    • Leonardo, aliyempoteza baba yake, anakumbuka jambo fulani lililompa nguvu na kumfariji. Alikuwa amerudi tu nyumbani, na alipokumbuka kwamba hakukuwa na mtu, alianza kulia sana. Alienda kwenye bustani iliyo karibu, akaketi kwenye benchi, na kuendelea kulia. Huku akilia, alimsihi Mungu amsaidie. Ghafula, gari likasimama na Leonardo akatambua kwamba lilikuwa likiendeshwa na ndugu yake Mkristo. Ndugu huyo alikuwa akisafirisha vitu na alikuwa ametumia njia ambayo hakukusudia. Kwa kumwona tu, Leonardo alifarijika.

  • Kukabiliana na Huzuni
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 1
    • Baada ya kumpoteza baba yake, Leonardo aliamua kujifunza lugha ya ishara ili ashiriki pamoja na viziwi ujumbe wa Biblia wenye kufariji. Amegundua kwamba jitihada zake za kuwasaidia viziwi zimemsaidia sana. Anasema: “Jambo moja ambalo limenisaidia kukabiliana na huzuni yangu ni tamaa ya kuwasaidia viziwi wajifunze kumhusu Mungu. Ninatumia wakati na nguvu nyingi kuwasaidia. Hisia zangu za huzuni ziligeuka kuwa za shangwe nilipomwona mwanafunzi wangu wa Biblia wa kwanza akibatizwa! Kwa kweli, kwa mara ya kwanza tangu baba yangu afe, nilijihisi nikiwa mwenye furaha sana.”—Matendo 20:35.

  • Kukabiliana na Huzuni
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 1
    • Leonardo anawazia baba yake akiwa hai tena katika ulimwengu mpya ulioahidiwa na Mungu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki