-
Ni nani aliyebuni kwanza?Uhai—Ulitokana na Muumba?
-
-
Kuiga mabawa ya shakwe-bahari
Shakwe-bahari hagandi kamwe, hata anaposimama kwenye barafu. Kiumbe huyo huhifadhi jinsi gani joto la mwili wake? Siri moja ni maumbile yake ya ajabu ambayo wanyama wengi wanaoishi maeneo yenye baridi kali huwa nayo. Maumbile hayo humwezesha kunururisha joto kinyume cha mkondo.
Heat transfers, remains in the body. Cold stays in the feet
Unururishaji-joto kinyume cha mkondo ni nini? Ili kuelewa wazo hilo, wazia mabomba mawili ya maji yaliyofungwa pamoja. Bomba moja linapitisha maji ya moto, na lile lingine linapitisha maji baridi. Ikiwa maji ya moto na maji baridi yanatiririka kuelekea upande mmoja, karibu nusu ya joto la maji ya moto litahamia kwenye maji baridi. Lakini, ikiwa maji ya moto na maji baridi yanatiririka kuelekea pande tofauti, karibu joto lote la maji ya moto litahamia kwenye maji baridi.
Shakwe-bahari anaposimama kwenye barafu, vinururishaji-joto kwenye miguu yake hupasha joto damu inaporudi kutoka kwenye miguu baridi ya ndege huyo. Vinururishaji-joto hivyo huhifadhi joto katika mwili wa ndege huyo na kuzuia lisipotee kupitia miguu yake. Arthur P. Fraas, mhandisi wa masuala ya ufundi na usafiri wa ndege, aliufafanua ubuni huo kuwa “mojawapo ya unururishaji-joto unaojifanyiza tena na wenye matokeo zaidi ulimwenguni.”13 Ubuni huo ni wa hali ya juu sana hivi kwamba wanadamu wameuiga.
-