-
Jinsi Hana Alivyopata AmaniMnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
-
-
Kadiri muda unavyopita, Hana hamsahau Samweli kamwe. Maandiko yanasema: “Mama yake alikuwa akimfanyizia koti dogo lisilo na mikono, na kumletea mwaka baada ya mwaka alipopanda pamoja na mume wake ili kutoa dhabihu ya kila mwaka.” (1 Samweli 2:19) Kwa kweli Hana anaendelea kusali kwa ajili ya Samweli. Bila shaka, kila mwaka anapomtembelea Samweli, Hana anamtia moyo aendelee kuwa mwaminifu katika kumtumikia Mungu.
-
-
Jinsi Hana Alivyopata AmaniMnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
-
-
Elkana na Hana ni mifano mizuri kama nini kwa wazazi Wakristo! Akina mama na baba wengi wamekuwa tayari kumwazima Yehova wana na binti zao, kwa njia ya mfano, kwa kuwahimiza wafuatilie aina fulani ya utumishi wa wakati wote mbali na nyumbani. Wazazi wenye upendo kama hao wanastahili kupongezwa kwa dhabihu wanazotoa. Na Yehova atawapa thawabu.
-