-
Jitihada ya Kutafuta FurahaMnara wa Mlinzi—2004 | Septemba 1
-
-
Jitihada ya Kutafuta Furaha
MIAKA michache iliyopita, watu nchini Marekani, Ufaransa, Uingereza, na Ujerumani waliulizwa, “Ni nini kinachohitajiwa ili kuwa na furaha?” Kati ya wale waliohojiwa, asilimia 89 walisema kwamba ni lazima uwe na afya nzuri; asilimia 79 wakataja ndoa au uhusiano mzuri; asilimia 62 wakataja thawabu ya kuwa mzazi; nao asilimia 51 wakasema kwamba ni lazima mtu awe na kazi nzuri ili awe na furaha. Na hata ingawa kwa kawaida watu wengi wanafundishwa kwamba pesa haziwezi kuleta furaha ya kudumu, asilimia 47 ya wale waliohojiwa walisadiki kwamba zinaweza.
-
-
Jitihada ya Kutafuta FurahaMnara wa Mlinzi—2004 | Septemba 1
-
-
Ni muhimu kuona kwamba uchunguzi uliotajwa mwanzoni mwa makala hii pia ulionyesha kwamba watu 4 kati ya 10 walihisi kwamba furaha hutokana na kuwafanyia wengine mema na kuwasaidia. Na mtu 1 kati ya 4 alikazia kwamba imani na usadikisho wa kidini ni muhimu sana ili kuwa na furaha.
-