Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Na juu ya kipaji cha uso wake paliandikwa jina, fumbo: ‘Babuloni Mkubwa, mama ya makahaba na ya vitu vya kunyarafisha vya dunia.’

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 17:4-

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 23. Ni jina gani kamili la Babuloni Mkubwa, na maana yalo ni nini?

      23 Kama ilivyokuwa desturi katika Roma ya kale, malaya huyu anatambuliwa kwa jina lililo juu ya kipaji cha uso wake.d Ni jina refu: “Babuloni Mkubwa, mama ya makahaba na ya vitu vya kunyarafisha vya dunia.” Jina hilo ni “fumbo,” jambo fulani lenye maana iliyofichwa. Lakini kwa wakati wa Mungu fumbo hilo litafafanuliwa. Kwa kweli, malaika anampa Yohana habari ya kutosha kuruhusu watumishi wa Yehova leo wafahamu umaana kamili wa jina hili lenye maelezo. Sisi tunatambua Babuloni Mkubwa kuwa dini bandia yote. Yeye ndiye “mama ya makahaba” kwa sababu dini bandia zote moja moja katika ulimwengu, kutia ndani mafarakano katika Jumuiya ya Wakristo, ni kama mabinti wake, zikimwiga yeye katika kufanya ukahaba wa kiroho.

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 25. (a) Ni nini kinachofananishwa na “kikombe cha dhahabu ambacho kilijaa vitu vya kunyarafisha?” (b) Ni katika maana gani kahaba wa ufananisho amelewa?

      25 Tazama sasa alicho nacho kahaba huyu mkononi mwake. Haikosi Yohana alitweta kwa mshangao kukiona—kikombe cha dhahabu “kimejaa vitu vya kunyarafisha na vitu visivyo safi vya uasherati wake”! Hiki ndicho kikombe ambacho ndani yacho mna “divai ya kasirani ya uasherati wake” ambacho kwa hicho amefanya mataifa yote yalewe. (Ufunuo 14:8; 17:4) Kwa nje kinaonekana kuwa chenye utajiri, lakini yaliyomo ni yenye kunyarafisha, si safi. (Linga Mathayo 23:25, 26.) Ndani kina mazoea yote machafu na uwongo mwingi ambao huyo kahaba mkubwa ametumia kutongoza mataifa na kuwaleta chini ya uvutano wake.

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 238]

      Chini ya kichwa hiki, makala inayofuata ilitokea katika chapa ya kwanza ya The New York Times ya Desemba 7, 1941:

      ‘SALA YA VITA’ KWA AJILI YA REICH

      Maaskofu wa Kikatoliki katika Fulda Waomba Baraka na Ushindi

      Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki wa Ujeremani lililokusanyika katika Fulda limependekeza ianzishwe ‘sala ya vita’ maalumu ambayo itasomwa mwanzoni na mwishoni mwa ibada zote za kimungu. Sala hiyo husihi Mungu abariki silaha za Ujeremani kwa ushindi na kutoa himaya kwa maisha na afya ya askari-jeshi wote. Maaskofu hao waliwaagiza zaidi makasisi wa Kikatoliki waweke na kukumbuka katika mahubiri maalumu ya Jumapili angalau mara moja kwa mwezi askari-jeshi Wajeremani ‘barani, baharini na hewani.’”

      Makala hii iliondolewa kwenye chapa za baadaye za nyusipepa hiyo. Desemba 7, 1941, ndiyo siku Japani, nchi fungamani na Ujeremani, iliposhambulia meli za U.S. kwenye Pearl Harbor.

      [Picha katika ukurasa wa 244]

      “Majina ya Kufuru”

      Hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alipoendeleza Ushirika wa Mataifa baada ya Vita ya Ulimwengu 1, hawara zake wa kidini walitafuta mara hiyo kulipa tendo hilo idhini ya kidini. Kama tokeo, tengenezo jipya la amani ‘likajawa na majina ya kufuru.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki