Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwalimu Mkuu Atudhihirishia Muumba Zaidi
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • Petro alijionea mtazamo wa Yesu wa kujali. Punde tu baada ya kujiunga na Yesu katika huduma, mama-mkwe wa Petro akawa mgonjwa kwa homa. Akija nyumbani kwa Petro, Yesu akamshika mama huyo kwa mkono, na homa ikaisha! Huenda tusijue hasa njia hiyo ya tiba, kama vile tu leo wanatiba hawawezi kueleza vizuri jinsi ambavyo baadhi ya tiba hutokea, lakini homa ilimwondoka mwanamke huyo. Jambo kubwa zaidi kuliko kujua njia yake ya tiba ni kuthamini kwamba kwa kuponya wagonjwa na wenye mapigo, Yesu alionyesha jinsi alivyowasikitikia. Kwa kweli alitaka kuwasaidia watu, na ndivyo ilivyo na Baba yake. (Marko 1:29-31, 40-43; 6:34) Kutokana na mambo aliyojionea akiwa na Yesu, Petro angeweza kuona kwamba Muumba amwona kila mtu kuwa astahili kutunzwa.—1 Petro 5:7.

  • Mwalimu Mkuu Atudhihirishia Muumba Zaidi
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • [Sanduku katika ukurasa wa 150]

      Huenda ukafurahia kulinganisha masimulizi yanayolingana ya jinsi Yesu alivyomponya mama-mkwe wa Petro. (Mathayo 8:14-17; Marko 1:29-31; Luka 4:38, 39) Tabibu Luka alitia ndani jambo la kitiba la kwamba huyo mama-mkwe alikuwa na “homa kali.” Ni nini kilichomwezesha Yesu amponye na kuponya wengine? Luka alikiri kwamba “nguvu ya Yehova ilikuwa hapo ili [Yesu] afanye uponyaji.”—Luka 5:17; 6:19; 9:43.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki