Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wakati Ambapo Ukubwa Haufai
    Amkeni!—1997 | Juni 22
    • Miongozo Mipya ya Uzito

      Serikali ya Marekani, ikiwa imesadikishwa kuhusu tatizo zito la uzito, ilikaza zaidi miongozo ya uzito iliyopendekezwa katika 1995. (Ona sanduku kwenye ukurasa ufuatao.) Miongozo iliyorekebishwa hutambulisha “uzito ufaao kiafya,” “uzito wa kupita kiasi kidogo,” na “uzito wa kupita kiasi sana.” Miongozo hiyo hutumika kwa wote watu wazima wanaume na wanawake, haidhuru umri wao ni upi.

      Miongozo ya 1990 iliandaa nafasi kwa ukuzi wa mwili wa katikati katika umri wa makamo, mara nyingi uitwao mpanuko wa umri wa makamo. Miongozo mipya haiandai nafasi hiyo, kwa kuwa inaonekana kwamba watu wazima hawapaswi kuongeza uzito kwa kuendelea.b Hivyo, mtu ambaye hapo awali alionwa kuwa wa uzito wa kawaida huenda akajipata katika kikundi cha wale wenye uzito wa kupita kiasi. Kwa kielelezo, mtu mwenye kimo cha sentimeta 168 kati ya umri wa miaka 35 na 65 ambaye alikuwa na uzito wa kilo 75 angekuwa katika kiwango cha uzito ufaao kiafya kulingana na miongozo ya 1990. Lakini katika miongozo mipya, yeye angekuwa na uzito wa kupita kiasi wa kilo tano!

  • Wakati Ambapo Ukubwa Haufai
    Amkeni!—1997 | Juni 22
    • Je, wewe uko katika sehemu ya “uzito ufaao kiafya,” “uzito wa kupita kiasi kidogo,” au “uzito wa kupita kiasi sana?” Grafu iliyoonyeshwa hapa itakusaidia kujibu swali hilo

      Miongozo ya Uzito ya 1995 kwa Wanaume na Vilevile Wanawake

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      Kimo *

      cm 198

      190

      180

      170

      160

      150

      kg 30 40 50 60 70 80 90 100 110

      Uzito†

      Takwimu zategemea: U.S. Department of Agriculture, U.S. Department of Health and Human Services

      *Bila viatu.

      †Bila nguo. Uzito wa juu zaidi watumika kwa watu walio na misuli na mifupa zaidi, kama ilivyo na wanaume wengi.

  • Wakati Ambapo Ukubwa Haufai
    Amkeni!—1997 | Juni 22
    • b Miongozo ya 1995 hutumika kwa vikundi vingi vya umri lakini si vyote. “Kuna mwafaka wa jumla kwamba miongozo mipya ya uzito yaelekea haitumiki kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65,” asema Dakt. Robert M. Russell katika jarida JAMA la Juni 19, 1996. “Uzito wa kupita kiasi kidogo tu katika mtu mwenye umri mkubwa zaidi waweza hata kunufaisha kwa kuandaa hifadhi ya nishati kwa vipindi vya ugonjwa na kwa kusaidia kuhifadhi misuli na tishu za mifupa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki