Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wewe Hula Vyema Kiroho?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 15
    • Sababu ya tatu ya sisi kuhitaji chakula, lasema gazeti Food and Nutrition, ni “kurekebisha afya ya mwili. . . na kuzuia maradhi.” Manufaa za kiafya za chakula kizuri hazionekani wazi mara moja. Tumalizapo mlo mzuri, ni mara chache tufikiriapo, ‘Mlo huo umenufaisha sana moyo wangu (au mafigo yangu au misuli yangu, na kadhalika).’ Hata hivyo, jaribu kutokula kwa kipindi fulani, na matokeo kwa afya yako yataonekana wazi. Matokeo gani? “Tokeo lililo la kawaida zaidi,” chasema kitabu cha marejezo ya kitiba, “ni lenye kudhuru: kushindwa kukua, kushindwa kukinza maambukizo madogo-madogo, ukosefu wa nishati au uanzisho.”

  • Je, Wewe Hula Vyema Kiroho?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 15
    • Kitabu cha mafundisho Food and Nutrition, kinachozungumzia umuhimu wa kuwa na mlo ufaao, chatupatia sababu nzuri tatu za kula vizuri. Sababu moja ni kwamba twahitaji chakula “ili kuendeleza ukuzi na kusawazisha kule kuharibika kwa chembe za mwili hatua kwa hatua.” Je, ulijua kwamba kila siku maishani mwako, trilioni moja ya chembe za mwili wako huharibika na mpya zahitaji kuchukua mahali pazo? Ukuzi na utunzi ufaao wa mwili wahitaji chakula kizuri.

  • Je, Wewe Hula Vyema Kiroho?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Aprili 15
    • Chakula chahitajiwa pia ili “kutokeza joto na nishati.” Chakula huandaa fueli ili miili yetu ifanye kazi vizuri. Ikiwa tunakula vibaya, tutakuwa na nishati kidogo. Upungufu wa madini ya chuma katika mlo wetu, waweza kutufanya tuhisi wachovu na walegevu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki