Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Njia ya 4—Linda Afya Yako
    Amkeni!—2011 | Machi
    • ◯ Dumisha usafi. “Kunawa mikono ndilo jambo moja muhimu unaloweza kufanya ili kuzuia kuenea kwa maambukizo na kuwa na afya na hali njema,” inasema ripoti ya Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa ya Kuambukiza vya Marekani. Asilimia 80 hivi ya maambukizo huenezwa kupitia mikono michafu. Kwa hiyo, nawa mikono mara nyingi iwezekanavyo kila siku. Fanya hivyo hasa kabla ya kutayarisha chakula, au kugusa au kusafisha kidonda, na pia baada ya kumgusa mnyama, kwenda msalani, au kumbadili mtoto nepi.

      Kunawa kwa kutumia sabuni ni bora kuliko kutumia kemikali za kuua viini zilizo na alkoholi. Watoto watakuwa na afya bora ikiwa wazazi watawazoeza kunawa mikono na kutogusa midomo na macho yao kwa mikono. Kuoga kila siku na kuwa na nguo na matandiko safi pia kutachangia kuwa na afya bora.

  • Njia ya 4—Linda Afya Yako
    Amkeni!—2011 | Machi
    • ◯ Hakikisha nyumba yako ni safi. Jitahidi sana kudumisha nyumba yako ikiwa nadhifu na safi, ndani na nje. Hakikisha kwamba maji hayajikusanyi mahali popote na hivyo kufanya mbu wazaane. Takataka, uchafu, na vyakula ambavyo havijafunikwa huvutia wadudu na wanyama wenye viini ambavyo husababisha magonjwa. Ikiwa hakuna choo, jenga choo cha shimo badala ya kwenda choo shambani. Funika shimo la choo ili kuzuia nzi ambao hupitisha maambukizo ya macho na magonjwa mengine.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki