Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kula Pamoja Kunaweza Kuimarisha Familia Yako?
    Amkeni!—2010 | Januari
    • Kula pamoja kama familia pia huwafanya watoto waishi maisha yenye usawaziko na yenye kuridhisha. Kituo cha Kitaifa cha Uraibu na Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya katika Chuo Kikuu cha Columbia huko Marekani, kiligundua kuwa watoto ambao hula na familia zao angalau mara tano kwa juma wana matatizo machache yanayohusishwa na mahangaiko, uchovu, au kukosa upendezi, na hata wao hupata maksi za juu shuleni.

  • Je, Kula Pamoja Kunaweza Kuimarisha Familia Yako?
    Amkeni!—2010 | Januari
    • Ni wazi kuwa kula pamoja kama familia kunaweza kuwasaidia kuepuka mazoea mabaya ya kula. Chuo Kikuu cha Navarre nchini Hispania kinaripoti kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo ya kula unapokula peke yako. Ni kweli kwamba matatizo hayo huenda yakatokea, lakini kukosa kula na wengine huongeza uwezekano wa kupatwa na matatizo hayo. “Inapokuwa jambo la kawaida kula pamoja, watoto huhisi kuwa wanapendwa. Kula pamoja huwafanya wahisi wakiwa salama kihisia kwa sababu ya mazingira yenye upendo katika familia,” anaeleza Esmeralda, mama ya binti wawili.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki