Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Utatembea Pamoja na Mungu?
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Novemba 1
    • Tunaweza Kutembeaje Pamoja na Mungu?

      9. Kwa nini nyakati nyingine Yehova alijificha kutoka kwa watu wake, lakini alitoa uhakikisho gani kwenye Isaya 30:20?

      9 Tunapaswa kuzingatia kwa makini swali la tatu. Nalo ni, Tunaweza kutembeaje pamoja na Mungu? Tunapata jibu katika andiko la Isaya 30:20, 21: “Mfundishaji wako Mkuu hatajificha tena, na macho yako yatakuwa macho yanayomwona Mfundishaji Mkuu wako. Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako likisema: ‘Hii ndiyo njia. Tembeeni ndani yake,’ iwe mtakwenda upande wa kuume au iwe mtakwenda upande wa kushoto.”

  • Je, Utatembea Pamoja na Mungu?
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Novemba 1
    • 10. Ni katika njia gani unaweza ‘kusikia neno nyuma yako’ kutoka kwa Mfundishaji wako Mkuu?

      10 Mstari wa 21 unaeleza mfano mwingine. Yehova anaelezwa kuwa anatembea nyuma ya watu wake akitoa mwongozo kuhusu njia inayofaa ya kutembea. Wasomi wa Biblia wameeleza kwamba maneno hayo yanahusiana na jinsi mchungaji nyakati nyingine anavyowafuata kondoo wake na kupaaza sauti ili kuwaongoza na kuwazuia wasipitie njia isiyofaa. Mfano huo unatuhusuje? Tunapotafuta mwongozo katika Neno la Mungu, tunasoma maneno yaliyoandikwa maelfu ya miaka iliyopita. Ni kana kwamba maneno hayo yanatoka nyuma yetu kwa sababu yaliandikwa zamani sana. Lakini yangali yanatufaa leo sawa na yalivyokuwa wakati yalipoandikwa. Shauri la Biblia linaweza kutuongoza katika maamuzi yetu ya kila siku na linaweza kutusaidia kupanga maisha yetu ya wakati ujao. (Zaburi 119:105) Tunapojitahidi kutafuta shauri hilo na kulitumia, Yehova anakuwa Kiongozi wetu. Hivyo, tunatembea pamoja na Mungu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki