Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mkazo—“Muuaji wa Kichinichini”
    Amkeni!—1998 | Machi 22
    • [Maelezo ya Chini]

      a Ingawa mkazo unaweza kuwa mojawapo ya mambo yenye kuchangia, katika visa vingi vya mshiko wa moyo, huwa kuna madhara makubwa katika ateri za moyo ambayo hutokezwa na mrundamano wa vitu vyenye mafuta-mafuta katika ateri. Kwa hiyo, si jambo la hekima kwa mtu kuchukua dalili za maradhi ya moyo kijuujuu tu, labda akiamini kwamba kupunguza tu mkazo kutamponyesha. Ona Amkeni!, Desemba 8, 1996, ukurasa wa 3-13.

  • Mkazo—“Muuaji wa Kichinichini”
    Amkeni!—1998 | Machi 22
    • “Dalili ya kwanza niliyoona ilikuwa msongo mkubwa sana. Msongo huo ulianzia karibu na mfupa wangu wa kidari; ukaenea haraka kwenye mabega yangu, shingo, na taya; na kuenea haraka tena kwenye mikono yangu yote miwili. Nilihisi kana kwamba tembo alikuwa amerukaruka kwenye kifua changu. Karibu nishindwe kupumua. Nikaanza kutoka jasho. Nilianza kushikwa na mipindo ya matumbo na kisha kichefuchefu kibaya sana. . . . Baadaye, wauguzi walipokuwa wakisaidia kuniweka kitandani katika hospitali, nakumbuka nikisema kwa mshangao, ‘Ninapatwa na mshiko wa moyo.’ Nilikuwa na umri wa miaka arobaini na nne.”

      HIVYO ndivyo Dakt. Robert S. Eliot afafanuavyo jinsi alivyonusurika kifo zaidi ya miaka 20 iliyopita katika kitabu chake From Stress to Strength. Mapema asubuhi hiyo alikuwa amehudhuria mkutano mmoja na alikuwa ametoa hotuba—na kwa kushangaza, ilikuwa juu ya habari ya mishiko ya moyo. Kwa ghafula, Dakt. Eliot, ambaye ni mtaalamu wa moyo, alijikuta akiwa ndiye “mgonjwa katika chumba cha utunzaji cha matatizo ya moyo.” Anasema ni nini kilichochangia tatizo lake ambalo halikutazamiwa? “Ndani ya mwili,” asema Dakt. Eliot, “jinsi nilivyokuwa nikiitikia mkazo ilikuwa ikiniua.”a

      Kama ambavyo mambo ya Dakt. Eliot yanavyoonyesha, mkazo waweza kutokeza hali zenye kutisha uhai. Kwa kweli, nchini Marekani, umehusianishwa na baadhi ya visababishi vikubwa zaidi vya kifo. Matokeo ya mkazo yaweza kuongezeka bila kutambuliwa katika kipindi fulani cha wakati kisha yatokee kwa ghafula. Kwa hiyo, ni kwa sababu nzuri kwamba mkazo umeitwa “muuaji wa kichinichini.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki