-
Kitu Chenye Thamani Kuliko KaziAmkeni!—2011 | Juni
-
-
Katika mwaka wa 1997, wakati Pavel, mwenye umri wa mwaka moja kutoka jiji la Novosibirsk alipohitaji upasuaji mara moja, mama yake aliwasiliana nasi ili kupata msaada. Wakati huo, nchini Urusi, kulikuwa na madaktari wachache tu wenye uzoefu ambao wangekubali kufanya upasuaji bila kutumia damu. Tulikubali kumsaidia kupata daktari ambaye angetumia matibabu ya badala.
Tulipata hospitali ya upasuaji wa moyo huko Kazan’ iliyokuwa na madaktari ambao walikubali kumfanyia Pavel upasuaji. Machi 31, 1997 (31/3/1997), walifaulu kumfanyia upasuaji wa kurekebisha tatizo baya la moyo linaloitwa tetralogy of Fallot bila kutumia damu. Mnamo Aprili 3 (3/4/1997), gazeti Vechernyaya Kazan, liliripoti hivi: “Kijana huyo mdogo yuko sawa na hahitaji tena kutumia dawa za moyo . . . Mama ya Pavlik [jina Pavel limenyambuliwa kuonyesha alikuwa mdogo] alitulia kwa mara ya kwanza katika muda wa miezi 11.” Baada ya muda mfupi, Pavel alipata nafuu baada ya upasuaji na akaanza kutembea akiwa bado hospitalini.
Pavel sasa ana afya nzuri na anaishi maisha ya kawaida. Anapenda kuogelea, kuteleza kwenye theluji, na kucheza kandanda. Yuko katika darasa la nane, na yeye pamoja na mama yake wanashirikiana na kutaniko moja la Mashahidi wa Yehova katika jiji la Novosibirsk. Baada ya kisa hicho, madaktari katika hospitali hiyo walifaulu kuwafanyia upasuaji wa moyo wagonjwa kadhaa ambao ni Mashahidi wa Yehova bila kutumia damu.
-
-
Kitu Chenye Thamani Kuliko KaziAmkeni!—2011 | Juni
-
-
[Picha katika ukurasa wa 15]
Pavel na mama yake leo
-