-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha DanieliMnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 1
-
-
1:11-15—Je, sura za vijana wanne wa Yudea zilikuwa nzuri sana kwa sababu ya chakula cha mboga za majani? Hapana. Hakuna chakula kinachoweza kutokeza mabadiliko hayo kwa siku kumi tu. Yehova ndiye aliyesababisha mabadiliko hayo ya sura za vijana hao Waebrania. Aliwabariki kwa sababu walimtumaini.—Methali 10:22.
-
-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha DanieliMnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 1
-
-
1:10-12. Danieli alielewa kwa nini “ofisa mkuu wa makao ya mfalme” alimwogopa mfalme naye akaacha kutoa ombi lake kwa ofisa huyo. Hata hivyo, baadaye Danieli alimwendea “mlinzi,” ambaye angeweza kukubali kwa urahisi ombi lake. Tunaposhughulika na hali ngumu, tunapaswa kutenda kwa ufahamu, uelewaji, na hekima kama hiyo.
-
-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha DanieliMnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 1
-
-
3:16-18. Inaelekea kwamba wale Waebrania watatu hawangejibu kwa uthabiti hivyo ikiwa tayari walikuwa wameshindwa na jaribu la chakula. Sisi pia tunapaswa kujitahidi kuwa “waaminifu katika mambo yote.”—1 Timotheo 3:11.
-