Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mahujaji na Wapuriti Walikuwa Nani?
    Amkeni!—2006 | Februari
    • Baada ya muda, makasisi Wapuriti walianza kufundisha kuhusu toba. Walionya kwamba ingawa Mungu ni mwenye rehema, wote walioasi sheria zake wangeenda moja kwa moja motoni. Makasisi hao walifundisha kwa mkazo kuhusu moto wa mateso ili wafuasi watii sheria. Pindi moja, mhubiri Jonathan Edwards wa karne ya 18 alizungumza kuhusu “Watenda Dhambi Mkononi mwa Mungu Mwenye Hasira.” Ufafanuzi wake wa moto wa mateso ulikuwa wenye kuogopesha sana hivi kwamba makasisi wengine walihitaji kutuliza hisia za kutaniko lililovurugika baada ya kusikia mahubiri hayo.

  • Mahujaji na Wapuriti Walikuwa Nani?
    Amkeni!—2006 | Februari
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 13]

      WAPURITI NA MOTO WA MATESO

      Mahubiri ya Wapuriti kuhusu moto wa mateso yalipingana na Neno la Mungu. Biblia inafundisha kwamba wafu hawajui jambo lolote, hawawezi kuhisi uchungu au kufurahi. (Mhubiri 9:5, 10) Isitoshe, wazo la kuwatesa watu halijawahi ‘kuingia moyoni’ mwa Mungu wa kweli. (Yeremia 19:5; 1 Yohana 4:8) Yeye huwasihi watu wabadili maisha yao, naye hashughuliki kwa ukatili na wakosaji wasiotubu. (Ezekieli 33:11) Tofauti na ukweli huo wa Maandiko, mara nyingi wahubiri wa dini ya Wapuriti walimfanya Mungu aonekane kuwa mkatili na asiye na fadhili. Pia walifanya watu wasiwe na huruma kwa kuwachochea watumie nguvu kuwanyamazisha wapinzani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki