Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kukua Katika Ujuzi Sahihi Juu ya Kweli
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika 1903 alitolewa mwito wa kushindana kwenye mjadala wa hadhara. Hali ya wafu lilikuwa mojapo masuala katika mfululizo uliotokea wa mijadala kati ya C. T. Russell na Dakt. E. L. Eaton aliyetumikia akiwa msemaji wa muungano usio rasmi wa wahudumu Waprotestanti katika sehemu ya magharibi ya Pennsylvania.

      Wakati wa mijadala hiyo Ndugu Russell alitegemeza imara hoja ya kwamba “kifo ni kifo, na kwamba wapendwa wetu, wafapo, kwa kweli wamekufa, kwamba hawako hai wala pamoja na malaika wala pamoja na roho waovu katika mahali pasipo na tumaini.” Ili kuunga mkono hilo, yeye alirejezea maandiko kama vile Mhubiri 9:5, 10; Warumi 5:12; 6:23; na Mwanzo 2:17. Yeye alisema hivi pia: “Maandiko yanapatana kabisa na yale ambayo wewe na mimi na mtu mwingine yeyote mwenye akili timamu, mwenye kusababu ifaavyo katika ulimwengu atakubali kuwa ndio utu wenye kupatana na akili na wenye kufaa wa Mungu wetu. Ni nini lijulishwalo kuhusu Baba yetu wa mbinguni? Kwamba yeye ni mwenye haki, kwamba yeye ni mwenye hekima, kwamba yeye ni mwenye upendo, kwamba yeye ni mwenye nguvu. Watu wote Wakristo watakiri sifa hizo za utu wa kimungu. Ikiwa ni hivyo, je, sisi twaweza kupata maana yoyote ya neno ambamo tungeweza kumfikiria Mungu kuwa mwenye haki na bado aadhibu kiumbe [aliyeumbwa kwa] mkono Wake kwa umilele wote, haidhuru dhambi yake ilikuwa nini? Mimi si mteteaji wa dhambi; wala siishi katika dhambi mimi mwenyewe, na mimi sihubiri dhambi kamwe. . . . Lakini nakuambia kwamba watu hawa wote waliopo hapa ambao ndugu yetu [Dakt. Eaton] asema wanasema bila staha kwa makufuru yao kwa Mungu na jina takatifu la Yesu Kristo wote ni watu ambao wamefundishwa fundisho hilo la mateso ya milele. Na wauaji-kimakusudi, wevi na watenda maovu wote waliomo gerezani, wote walifundishwa fundisho hilo. . . . Hayo ni mafundisho mabaya; yamekuwa yakidhuru ulimwengu kwa muda wote huu; hayo si sehemu ya fundisho la Bwana hata kidogo, na uwezo wa kuona wa kiroho wa ndugu yetu mpendwa ungali una giza.”

      Inaripotiwa kwamba baada ya mjadala huo, kasisi mmoja aliyehudhuria alimwendea Russell na kusema: “Naterema kuona ukielekeza bomba la maji kwenye helo na kuuzima moto huo.”

  • Kukua Katika Ujuzi Sahihi Juu ya Kweli
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 128]

      Katika mjadala wa hadhara, Russell alitoa hoja kwamba wafu ni wafu kabisa, wala hawako hai pamoja na malaika wala pamoja na roho waovu katika mahali pasipo na tumaini

      Jumba la Carnegie, Allegheny, Pennsylvania—mahali mjadala ulipofanyiwa

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki