-
Herode Mkuu—Mjenzi StadiAmkeni!—2009 | Septemba
-
-
Yerusalemu na Hekalu la Herode
Mradi mkubwa zaidi wa Herode ulikuwa ujenzi wa hekalu la Yerusalemu. Hekalu la awali lilijengwa na Mfalme Sulemani, ambaye alifuata ramani za ujenzi za baba yake Daudi, ambaye alizipokea kutoka kwa Mungu. (1 Wafalme 6:1; 1 Mambo ya Nyakati 28:11, 12) Hekalu hilo liliharibiwa na Wababiloni miaka 420 hivi baadaye, na miaka 90 hivi baadaye, mahali pake palichukuliwa na jengo lisilo la kifahari sana lililojengwa na Gavana Zerubabeli wa Yuda.
Yosefo aliandika hivi kuhusu hekalu ambalo Herode alijenga mahali hapo: Lilikuwa “limefunikwa pande zote kwa mabamba makubwa ya dhahabu, punde tu jua lilipochomoza, hekalu hilo liliangaza sana hivi kwamba watu waliojaribu kulitazama walilazimika kufunika macho yao, kana kwamba walikuwa wakimulikwa na jua lenyewe. Kwa umbali wageni waliliona kuwa kama mlima uliofunikwa kwa theluji; kwa kuwa chochote ambacho hakikufunikwa kwa dhahabu kilikuwa cha rangi nyeupe pepepe.”
Maelfu ya watu walishiriki katika ujenzi wa kuta za hekalu, ambazo kwenye upande wa magharibi zilikuwa na urefu wa mita 500 hivi. Hayo mawe makubwa hayakuunganishwa kwa saruji. Jiwe moja lilikuwa na uzito wa tani 400 hivi na kulingana na msomi mmoja “hakuna mawe mengine yanayoweza kulinganishwa nayo kwa ukubwa katika ulimwengu huo wa kale.” Si ajabu kwamba wanafunzi wa Yesu walistaajabu! (Marko 13:1) Zaidi ya kuta hizo kulikuwa na jukwaa kubwa lililoitwa Eneo la Hekalu la Mlimani, ambalo ndilo jukwaa kubwa zaidi lililojengwa katika ulimwengu wa kale. Ukubwa wa jukwaa hilo ulikuwa sawa na zaidi ya viwanja 25 vya mpira.
-
-
Herode Mkuu—Mjenzi StadiAmkeni!—2009 | Septemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 25]
HEKALU LA HERODE
Mfano
-