-
No Help From This WorldUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
18. Rabshake ampa Hezekia onyo gani?
18 Wafalme wa Ashuru waliisifu miungu yao kutokana na ushindi vitani. Kitabu kiitwacho Ancient Near Eastern Texts kina maandishi ya Ashurbanipali, mtawala Mwashuri aliyedai kuwa aliongozwa “na miungu mikuu iitwayo Ashuru, Beli, Nebo, ambayo ilikuwa mabwana wake, waliotembea kando yake sikuzote, alipowashinda wanajeshi waliozoea vita . . . katika pigano kubwa.” Katika siku ya Isaya, Rabshake, anayewakilisha Mfalme Senakeribu wa Ashuru, aonyesha itikadi hiyo katika hotuba yake kwa Mfalme Hezekia kwamba miungu inahusika katika vita vya binadamu. Amwonya mfalme wa Wayahudi kwamba asiutegemee wokovu wa Yehova naye aeleza kwamba miungu ya mataifa mengine haikuweza kuwalinda watu wake dhidi ya jeshi lenye nguvu la Ashuru.—2 Wafalme 18:33-35, kielezi-chini.
19. Hezekia aitikiaje dhihaka za Rabshake?
19 Mfalme Hezekia aitikiaje? Masimulizi ya Biblia yasema: “Mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya BWANA.” (2 Wafalme 19:1) Hezekia atambua kwamba kuna Mmoja tu awezaye kumsaidia katika hali hiyo yenye kutia woga. Yeye ajinyenyekeza na kuutegemea mwelekezo wa Yehova.
20. Yehova atatendaje kwa niaba ya wakazi wa Yuda, nao wapaswa kujifunza nini kutokana na hilo?
20 Yehova atoa mwelekezo ambao umeombwa. Kupitia nabii Isaya, yeye asema: “Katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu.” (Isaya 31:7) Yehova awapiganiapo watu wake, miungu ya Senakeribu itathibitishwa kuwa isiyofaa kitu. Wakazi wa Yuda wapaswa kuzingatia fundisho hilo. Licha ya uaminifu wa Mfalme Hezekia, nchi ya Yuda, sawa na Israeli, imejazwa sanamu. (Isaya 2:5-8) Itahitaji wakazi wa Yuda wasitawishe uhusiano wao na Yehova kwa kutubu dhambi zao na kukataa ‘kila mtu sanamu zake.’—Ona Kutoka 34:14.
21. Isaya aelezaje kwa unabii matendo ya hukumu ya Yehova dhidi ya Mwashuri?
21 Isaya sasa aeleza kwa unabii matendo ya hukumu ya Yehova dhidi ya adui ya Yuda mwenye kutia hofu: “Huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.” (Isaya 31:8) Wakati wa kupambana ufikapo, wakazi wa Yerusalemu hawatahitaji hata kidogo kuchomoa panga zao kutoka alani mwake. Wanajeshi bora katika jeshi la Ashuru waangamizwa, si kwa panga za binadamu, bali kwa upanga wa Yehova. Mfalme Senakeribu wa Ashuru naye “ataukimbia upanga.” Baada ya wapiganaji wake 185,000 kufa mikononi mwa malaika wa Yehova, yeye arudi nyumbani. Baadaye, wanawe wamwua anapokuwa akiinamia Nisroki mungu wake.—2 Wafalme 19:35-37.
22. Wakristo leo waweza kujifunza nini kutokana na matukio yaliyohusisha Hezekia na jeshi la Ashuru?
22 Hakuna mtu yeyote, akiwemo Hezekia, ambaye angeweza kuona kimbele jinsi ambavyo Yehova angekomboa Yerusalemu kutoka kwa jeshi la Ashuru. Hata hivyo, njia ya Hezekia ya kushughulikia mgogoro huo yaandaa kielelezo bora kwa wale walio na majaribu leo. (2 Wakorintho 4:16-18) Kwa kuzingatia sifa yenye kuogopesha ya Waashuri wanaotishia Yerusalemu, yaeleweka ni kwa nini Hezekia anahofu. (2 Wafalme 19:3) Licha ya hayo, yeye alikuwa na imani katika Yehova, na akatafuta mwongozo Wake, wala si wa mwanadamu. Kufanya hivyo kulikuwa baraka iliyoje kwa Yerusalemu! Huenda Wakristo wenye kumhofu Mungu leo wakapata hisia kali chini ya mkazo. Katika hali nyingi, yaeleweka ni kwa nini watu wanaweza kuhofu. Ingawa hivyo, ‘tukitupa hangaiko letu lote juu ya Yehova,’ atatutunza. (1 Petro 5:7) Atatusaidia tuishinde hofu yetu naye atatuimarisha ili tukabiliane na hali inayoleta mkazo.
-
-
No Help From This WorldUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
[Picha katika ukurasa wa 326]
Hezekia alienda nyumbani kwa Yehova kutafuta msaada
-