Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nabii wa Mungu Awaletea Wanadamu Nuru
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Kulikuwa na “Isaya” Wangapi?

      7. Wasomi wengi wameutiliaje shaka uandikaji wa Isaya, na kwa nini?

      7 Unabii ni jambo moja ambalo limefanya wasomi wengi watilie shaka uandikaji wa Isaya. Hao wakosoaji hushikilia kwamba sehemu ya mwisho ya kitabu hicho bila shaka iliandikwa na mtu wa karne ya sita K.W.K., ama wakati wa uhamisho Babiloni ama baadaye. Maoni yao ni kwamba unabii mbalimbali wa ukiwa wa Yuda uliandikwa baada ya kutimizwa, na basi haukuwa utabiri kamwe. Wao husema pia kwamba baada ya sura ya 40, kitabu cha Isaya huongea kana kwamba serikali kuu wakati huo ilikuwa Babiloni na Waisraeli walikuwa watekwa huko. Kwa hiyo wanasababu kwamba hakuna shaka kuwa yeyote yule aliyeandika sehemu ya mwisho ya Isaya aliiandika wakati huo—karne ya sita K.W.K. Je, kusababu huko kuna msingi mzuri? Hata kidogo!

      8. Kutilia shaka uandikaji wa Isaya kulianza lini, na kulieneaje?

      8 Karne ya 12 W.K. ilipofika, hapo ndipo uandikaji wa Isaya ulipoanza kutiliwa shaka. Ulitiliwa shaka na mwelezaji Myahudi Abraham Ibn Ezra. Kichapo Encyclopaedia Judaica husema kwamba “katika maelezo yake juu ya Isaya, [Abraham Ibn Ezra] anasema kwamba ile nusu ya pili, kuanzia sura ya 40, ni maandishi ya nabii aliyeishi wakati wa Uhamisho wa Babiloni na mapema baada ya Kurudi Sayuni.” Katika karne ya 18 na ya 19, maoni ya Ibn Ezra yalifuatwa na wasomi kadhaa, mmoja wao akiwa Johann Christoph Doederlein, mtaalamu wa dini Mjerumani aliyechapisha kitabu cha kufafanua Isaya mwaka wa 1775, kukiwa na chapa ya pili mwaka wa 1789. Kichapo New Century Bible Commentary husema hivi: “Sasa wasomi wote, isipokuwa wale wanaoshikilia maoni yao, wanakubaliana na fikira ya Doederlein . . . kwamba unabii mbalimbali unaopatikana katika sura ya 40 mpaka ya 66 katika kitabu cha Isaya si maneno ya nabii Isaya wa karne ya nane, bali ulitokea baadaye.”

      9. (a) Kitabu cha Isaya kimegawanywaje? (b) Mwelezaji mmoja wa Biblia anatoaje muhtasari wa ubishi unaohusu uandikaji wa Isaya?

      9 Hata hivyo, maswali kuhusu uandikaji wa kitabu cha Isaya hayakuishia hapo. Fikira ya kwamba kulikuwa na Isaya wa pili ilianzisha wazo la kwamba huenda ikawa kulikuwa na mwandishi wa tatu.a Kisha kitabu cha Isaya kikazidi kugawanywa, hivi kwamba msomi mmoja anasema sura ya 15 na ya 16 ziliandikwa na nabii asiyejulikana, huku mwingine akitilia shaka uandishi wa sura ya 23 mpaka ya 27. Bado mwingine anasema haiwezi kuwa ni Isaya aliyeandika maneno yaliyo katika sura ya 34 na ya 35. Kwa nini? Kwa sababu habari zilizomo zinafanana sana na zile za sura ya 40 mpaka ya 66, zilizokuwa tayari zimetajwa kuwa ziliandikwa na mtu mwingine wala si Isaya wa karne ya nane! Mwelezaji wa Biblia Charles C. Torrey anataja kwa ufupi matokeo ya kusababu hivyo. Anasema kwamba “Yule ‘Nabii wa Uhamishoni’ aliyekuwa mashuhuri amepoteza umashuhuri wake kabisa, na maandishi yake yamegawanywa ovyo kuwa vipande vipande.” Hata hivyo, si wasomi wote wanaokubaliana na ugawanyaji huo wa kitabu cha Isaya.

  • Nabii wa Mungu Awaletea Wanadamu Nuru
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Yule anayefikiriwa kuwa mwandishi wa tatu, na anayesemekana aliandika sura ya 56 mpaka ya 66, hutajwa na wasomi kuwa Isaya wa Tatu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki