Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Gospeli—Je, Ni za Kweli au Ni Hekaya Tu?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 15
    • Mwanahistoria Will Durant aandika hivi katika kitabu chake Caesar and Christ: “Kwamba wanaume wachache wa kawaida wangeweza . . . kubuni mtu mwenye nguvu na mwenye uvutano mwingi kadiri hiyo, mwenye maadili ya hali ya juu kadiri hiyo na mtu mwenye kuonyesha ubinadamu sana kwa kadiri hiyo, ungekuwa muujiza wenye kustaajabisha mno zaidi ya wowote ulioandikwa katika Gospeli. Baada ya Biblia kuchambuliwa kwa muda wa karne mbili, maelezo yanayohusu maisha, tabia, na mafundisho ya Kristo yanabaki yakiwa wazi vya kutosha, na ndiyo sehemu yenye kusisimua zaidi katika historia ya watu wa Magharibi.”

  • Gospeli—Je, Ni za Kweli au Ni Hekaya Tu?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 15
    • Mwanahistoria Durant alichunguza masimulizi ya Gospeli akiwa na lengo zuri kabisa—yakiwa maandishi ya historia. Japo anasema kwamba kuna mambo yanayoonekana kana kwamba yanapingana, akata kauli hivi: “Ni mambo madogo-madogo yanayopingana, wala si mambo muhimu; katika mambo ya msingi zile gospeli tatu za kwanza zakubaliana sana, na kutokeza Kristo mwenye utu uleule.”

  • Gospeli—Je, Ni za Kweli au Ni Hekaya Tu?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 15
    • Vipi juu ya madai ya wahakiki wa Biblia kwamba Gospeli hazifikii viwango vya kuthibitishia historia halisi? Durant aendelea kusema: “Kutokana na shauku ya kuvumbua mambo, Uhakiki wa Biblia umetumia kanuni ngumu sana za kuthibitishia uasilia wa Agano Jipya hivi kwamba kanuni hizo zikitumiwa kwingineko basi mamia ya watu mashuhuri wa nyakati za kale—kama Hamurabi, Daudi, na Sokrate—wangeonwa kuwa hekaya tu. Japo upendeleo wa waevanjeli hao na mawazo waliyoshikilia ya kitheolojia, wao wamerekodi matukio mengi ambayo wabuni tu [wa hekaya] wangeficha—kama yale mashindano baina ya mitume ya kutaka ukubwa katika Ufalme, jinsi walivyotoroka baada ya Yesu kukamatwa, na jinsi Petro alivyomkana . . . Hakuna mtu yeyote anayesoma mambo hayo awezaye kutilia shaka ukweli wa mtu anayezungumziwa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki