Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Ungependa Kukutana na Fira?
    Amkeni!—1996 | Machi 22
    • Ibada ya Fira na Ushirikina

      IBADA ya fira imekuwako tangu nyakati za kale. Sanamu ya mfano wa fira imepatikana kwenye sili katika Mohenjo-Daro, mojapo staarabu za kale sana ambazo zimepata kufukuliwa na waakiolojia. Toka mileani ya tatu K.W.K. kufikia sasa, mamilioni katika India wamewapa fira staha ya kishirikina. Kwa kupendeza, nyingi kati ya hadithi za fira zaweza kutambuliwa kuwa ngano zilizopotoshwa zenye msingi wa matukio halisi ya kihistoria.

      “Hadithi” ya uumbaji hueleza juu ya wakati ambapo hakukuwa na nuru katika ulimwengu wote mzima. Kutokana na maji meusi ya ulimwengu wote mzima mungu Vishnu aliumbwa kwanza, kisha mbingu, dunia, na ulimwengu wa chini. Kutokana na mabaki ya uumbaji, fira mkubwa sana aitwaye Shesha (ikimaanisha sehemu iliyobaki) aliumbwa. Ngano husema kwamba fira alikuwa na kati ya vichwa 5 hadi 1,000, nazo picha huonyesha Vishnu akiwa amemkalia Shesha aliyejipinda, akiwa chini ya himaya ya shela iliyo wazi ya vichwa vingi vya Shesha. Matetemeko ya dunia yasemwa kuwa ni tokeo la Shesha kupiga miayo, nao moto kutoka kinywani mwake au sumu yake huuharibu ulimwengu mwishoni mwa enzi fulani.

      Ngano za Kihindi husema juu ya jamii ya fira inayoitwa Nagas, ambao wanaishi katika ulimwengu wa chini, Nagalok au Patala. Sokwe-mungu Hanuman hudai kwamba katika “Enzi Kamilifu,” watu wote walikuwa watakatifu, kulikuwa na dini moja tu, na hakukuwa na roho waovu wala Nagas. Nyoka wakawa walinzi wa utajiri wa dunia nao wakapata ujuzi mwingi na nguvu za kufanya mambo ya ajabu. Shesha, ambaye huitwa Vasuki nyakati nyingine, alitumiwa na miungu kusukasuka bahari ya maziwa ili kutokeza amrit, umajimaji mtamu ambao ungempa mtu kutokufa. Ulimwengu wa chini, uliokuwa ukitawalwa na Nagas, waonyeshwa kuwa mahali penye kutamanika zaidi; askari wanaokufa vitani wanaahidiwa raha isiyowazika huko.

      Hata hivyo, si fira wote wa kingano wanaoonwa kuwa wenye fadhili. “Hadithi” moja hueleza juu ya kabiliano kati ya Krishna, aliyegeuka kutoka kwa Vishnu na Kaliya, fira-daimoni mkubwa, mwenye kufisha. Picha huonyesha Krishna mshindi akiwekelea mguu wake juu ya huyo nyoka mkubwa.

      Manasa, au Durgamma, malkia wa Nagas, huabudiwa na wanawake ili awalinde wana wao kutokana na kuumwa na nyoka. Katika msherehekeo wa Nagapanchami, wanaoabudu nyoka humwaga maziwa na hata damu juu ya mifano ya fira na ndani ya mashimo ya nyoka. Mifano ya fira ya mawe au fedha huabudiwa na kupewa kuwa toleo katika mahekalu na wanawake wakitarajia kupata watoto wa kiume.

  • Je, Ungependa Kukutana na Fira?
    Amkeni!—1996 | Machi 22
    • Sinema ya mambo hakika, Shakti, ilifanyizwa kwenye msherehekeo katika Rajasthan, India, ambako kila Agosti mamia ya maelfu ya waabudu-nyoka hukutana jangwani. Chini ya jua kali, na kwenye halijoto zifikiazo digrii 50 Sentigredi, wao hujitandika kwa fito za chuma na kutambaa kwa matumbo yao kwa zaidi ya kilometa mbili juu ya mchanga wenye kuchoma hadi hekaluni kwa mungu-nyoka, Gogha. Mfalme fulani wa kihistoria katika karne ya kumi W.K., Gogha asemekana kuwa aliwaokoa watu wake kutokana na washambulizi Waislamu kwa kumwongoza adui kwenye eneo lenye nyoka wengi, ambako wengi katika jeshi hilo walikufa kutokana na kuumwa na nyoka.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki