Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Waionaje Dhambi?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Julai 15
    • “HAKUNA dhambi ndani yako, hakuna taabu ndani yako; wewe ndiwe ghala ya uwezo wote.” Mwanafalsafa maarufu wa Kihindu Vivekananda alitoa taarifa hiyo alipokuwa akifafanua fungu fulani kutoka kitabu kitakatifu cha Wahindu, kiitwacho Bhagavad Gita. Akitaja falsafa ya Vedanta, yeye adai hivi: “Kosa lililo kubwa zaidi ya yote ni kusema kwamba wewe u dhaifu, kwamba wewe ni mtenda-dhambi.”a

      Je, hata hivyo, ni kweli, kwamba hakuna dhambi katika mwanadamu? Na ni nini, ikiwa kuna chochote, ambacho mtu hurithi, wakati wa kuzaliwa? “Vitabia vya kimwili [tu] ndivyo vinaamuliwa na urithi-tabia,” asema Nikhilananda, mwalimu wa Kihindu. Tabia nyingine zinaamuliwa na “matendo ya mtu katika maisha yake mbalimbali ya hapo awali.” Kulingana na Vivekananda, “wewe ndiwe mfanyiza wa mambo yatakayokupata hatimaye.” Dini ya Hindu haifundishi chochote juu ya dhambi iliyorithiwa.

  • Wakati Dhambi Haitakuwapo Tena
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Julai 15
    • “JE, SISI huzaliwa katika dhambi?” Swali hilo lilitatanisha mwanafunzi-mhitimu katika Marekani mara baada ya yeye kuanza kujifunza Biblia. Kwa sababu ya malezi yake ya Kihindu, wazo la dhambi iliyorithiwa lilikuwa geni kwake. Lakini ikiwa dhambi kwa kweli imerithiwa, alisababu, kukataa au kupuuza uhalisi wake, kungekuwa jambo lisilofaa. Je, mtu angeweza kupataje jibu kwa swali hilo?

      Ikiwa dhambi imerithiwa, lazima ilikuwa na mwanzo. Je, mwanadamu wa kwanza aliumbwa akiwa mbaya hivi kwamba aliwapokeza watoto wake vitabia viovu? Au hiyo kasoro ilijitokeza baadaye? Ni lini hasa dhambi ilianza? Kwa upande mwingine, ikiwa dhambi ni uovu ulio nje tu, au ni kanuni, je, tunaweza kweli kutumainia kupata kuokolewa kutoka hiyo?

      Kulingana na itikadi ya Kihindu, kuteseka na uovu ni viambata vya uumbaji. “Kuteseka [au uovu],” aandika msomi wa Kihindu, “kama baridi-yabisi yenye kudumu sana, hujongea tu kutoka mahali pamoja hadi pengine lakini hakuwezi kuondolewa kabisa.” Uovu umekuwa sehemu ya ulimwengu wa wanadamu katika historia yote iliyorekodiwa. Ikiwa uovu watangulia rekodi za kihistoria za mwanadamu, majibu yenye kutegemeka juu ya asili yao lazima kwa vyovyote yatokane na chanzo cha juu zaidi kuliko mwanadamu. Majibu lazima yatoke kwa Mungu.—Zaburi 36:9.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki