Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wapaswa Kuamini Katika Kutwaa Umbo Jipya?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • Utu wa Mungu na Sheria ya Karma

      “Sheria ya Karma,” akafafanua Mohandas K. Gandhi, “ni isiyobadilika na isiyoweza kuepukwa. Hivyo hakuna uhitaji wa Mungu kuingilia mambo. Aliiweka hiyo sheria na, kusema kitamathali, akastaafu.” Gandhi aliona ufafanuzi huo kuwa wenye kusumbua.

      Kwa upande mwingine, ahadi ya ufufuo hufunua kwamba Mungu anapendezwa sana na viumbe wake. Kumrudisha mfu kwenye uhai tena katika dunia iliyo paradiso, lazima Mungu ajue na kukumbuka kila jambo juu ya mtu huyo. Kwa kweli Mungu hujali kila mmoja wetu.—1 Petro 5:6, 7.

  • Je, Wapaswa Kuamini Katika Kutwaa Umbo Jipya?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • Hata hivyo, itikadi ya kutwaa umbo jipya ilipevuka kabisa huko India. Wenye hekima Wahindu walikuwa wakishindana na matatizo ya ulimwengu wote mzima ya uovu na ya kuteseka miongoni mwa wanadamu. ‘Hayo yaweza kupatanishwaje na dhana ya Muumba mwadilifu?’ waliuliza. Walijaribu kusuluhisha hitilafiano kati ya uadilifu wa Mungu na maafa yasiyotazamiwa na ukosefu wa usawa ulimwenguni. Hatimaye, walibuni “sheria ya karma,” sheria ya sababu na matokeo—‘chochote apandacho mtu, hicho ndicho atakachovuna.’ Walitayarisha ‘taarifa ya hali ya fedha’ yenye mambo yote ambamo faida na hasara katika mojawapo ya maisha zinathawabishwa au kuadhibiwa katika maisha yafuatayo.

      “Karma” humaanisha tu “tabia.” Mhindu husemwa kuwa ana karma nzuri ikiwa yeye hupatana na kawaida za kijamii na kidini na husemwa kuwa ana karma mbaya ikiwa hafanyi hivyo. Tabia, au karma yake, huamua wakati wake ujao katika kila kuzaliwa upya kunakofuata. “Watu wote huzaliwa wakiwa na programu ya utendaji wa kiutu, hasa wakiwa wametayarishwa na matendo yao katika maisha za awali, ingawa vitabia vyao vya kimwili huamuliwa na urithi,” asema mwana-falsafa Nikhilananda. “[Hivyo] mtu ni mbuni wa ajali yake mwenyewe, mjenzi wa tokeo lake mwenyewe la hatima.” Hata hivyo, mradi wa mwisho ni kuwekwa huru kutoka katika duru hiyo ya uhamaji na kuunganishwa na Brahman—uhalisi wa mwisho. Yaaminiwa kwamba hilo hufikiwa kwa kujitahidi kufikia tabia yenye kukubaliwa kijamii na ujuzi wa pekee wa Hindu.

      Hivyo fundisho la kutwaa umbo jipya hutumia fundisho la hali ya kutokufa kwa nafsi kuwa msingi walo nalo huliendeleza kwa kutumia sheria ya karma. Acheni tuone Neno la Mungu lililopuliziwa, Biblia, lina yapi ya kusema kuhusu mawazo hayo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki