Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Waamini Katika Kutwaa Umbo Jipya?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • “WAMKUMBUKA msichana jirani uliyemwonea shauku ya kipumbavu ulipokuwa ukikua hapa India?” Mukundbhai akamwandikia mwanaye, aliye mwanafunzi wa chuo kikuu huko Marekani. “Ataolewa baada ya majuma machache. Nilidhani wapaswa kujua.”

      Kwa nini huyo baba alimjulisha mwanaye habari hiyo? Kwa vyovyote, Mukundbhai alikomesha waziwazi mapenzi hayo ya utineja miaka mingi iliyopita. Isitoshe, huyo mwana alikuwa amekuwa Marekani akifuatia elimu ya juu kwa miaka sita. Hakuwa amewasiliana na huyo msichana wakati huo, na Mukundbhai alijua hilo.

      Mbona, basi, ahangaike? Alihangaika kwa sababu Mukundbhai aliamini katika kutwaa umbo jipya, au kuzaliwa upya.a Ikiwa kwa kutukia yale mapenzi ya utotoni kati yao wawili yalikuwa kwa sababu ya kuwa washirika katika maisha yao ya awali, ungekuwa ukatili kuwatenganisha sasa wakiwa na umri wa kutosha kufunga ndoa. Mukundbhai alitaka tu kumjulisha mwanaye juu ya hiyo hali kabla ya huyo msichana kuwa mke wa mtu mwingine katika maisha haya.

      Fikiria kisa kingine. Msichana mwenye umri wa miaka minne alikuwa amelazwa akiwa na maumivu makali mara kadha wa kadha katika hospitali fulani huko Mumbai, India. Tatizo lake lilikuwa mshipa wenye kasoro moyoni mwake. Wazazi wake matajiri walisononeshwa kumwona mtoto wao akiteseka. Lakini walisababu hivi: “Lazima tukubali jambo la hakika kwamba tuna mtoto asiye na afya nzuri. Lazima awe alifanya jambo fulani katika maisha yake ya awali ili astahili jambo hili.”

      Itikadi katika kutwaa umbo jipya ina fungu muhimu maishani mwa mamilioni ya watu walio katika Dini ya Hindu, Dini ya Buddha, Dini ya Jaini, Dini ya Sikh, na dini nyingine zilizoanzia India. Mambo yaliyoonwa maishani—kuanzia na kushikwa na mapenzi hadi kuteseka sana —yanaonwa kuwa matokeo ya matendo yaliyofanywa katika maisha ya awali au maisha za awali.

  • Je, Waamini Katika Kutwaa Umbo Jipya?
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • “Makumbukumbu ya maisha yaliyopita!” wasema wanaoamini katika kutwaa umbo jipya. Basi, Ratana mwenye umri wa miaka mitatu aliye Bangkok alipoanza kuwa na “makumbukumbu ya maisha yake yaliyopita akiwa mwanamke wa kidini aliyekufa katika miaka yake ya 60,” watazamaji walio wengi walikubali kisa chake kuwa ithibati halali ya kutwaa umbo jipya.

      Hata hivyo, kuna shaka. Na kwaweza kuwa na mafafanuzi mengine ya makumbukumbu yahesabiwayo maisha ya awali.b Katika kitabu chake Hinduism: Its Meaning for the Liberation of the Spirit, Nikhilananda, mwanafalsafa Mhindu asema kwamba ‘mambo yaonwayo baada ya kifo hayawezi kuthibitishwa kwa kufikiri.’ Hata hivyo anasisitiza kwamba “uwezekano wa fundisho la kuzaliwa upya ni mkubwa kuliko kutowezekana kwalo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki