Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya Kwanza
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
    • Je, Maandishi ya Wanahistoria wa Kale Ni Sahihi?

      Wanahistoria walioishi karibu na wakati ambapo jiji la Yerusalemu liliharibiwa wanatoa habari zinazotofautiana kuhusu wafalme wa Milki Mpya ya Babiloni.c (Ona sanduku “Wafalme wa Milki Mpya ya Babiloni.”) Mfuatano wao wa matukio haupatani na ule wa Biblia. Hata hivyo, maandishi yao yanategemeka kadiri gani?

      Mbabiloni anayeitwa Berossus, ambaye alikuwa “kuhani wa Beli,” ni mmoja kati ya wanahistoria walioishi karibu na kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni. Kitabu chake kinachoitwa Babyloniaca, ambacho aliandika yapata mwaka wa 281 K.W.K., kilipotea, na ni visehemu tu vya kitabu hicho ambavyo vimehifadhiwa katika maandishi ya wanahistoria wengine. Berossus alidai kwamba alitumia “vitabu ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa kwa uangalifu sana huko Babiloni.”1 Je, maandishi yake yalikuwa sahihi? Fikiria mfano mmoja.

      Berossus aliandika kwamba Mfalme Senakeribu wa Ashuru alitawala baada ya “ndugu [yake]”; na baada yake mwana wake [Esarhadoni akatawala kwa] miaka 8; kisha, Sammuges [Shamash-shuma-ukin] akatawala kwa miaka 21.” (Kitabu cha Tatu, 2.1, 4) Hata hivyo, hati za historia ya Babiloni zilizoandikwa muda mrefu kabla ya kipindi cha Berossus zinasema kwamba Senakeribu alitawala baada ya baba yake, Sargoni wa Pili, na si baada ya ndugu yake; Esarhadoni alitawala miaka 12, si miaka minane; naye Shamash-shuma-ukin akatawala miaka 20, si miaka 21. Ingawa msomi R. J. van der Spek, anakubali kwamba Berossus alichunguza maandishi ya mfuatano wa matukio ya Wababiloni, anaandika hivi: “Hilo halikumzuia kuongeza mambo yake na ufafanuzi wake.”2

      Wasomi wengine wana maoni gani kumhusu Berossus? “Zamani Berossus alionwa kuwa mwanahistoria,” anasema S. M. Burstein, ambaye alifanya uchunguzi wa kina kuhusu maandishi ya Berossus. Hata hivyo, alimalizia kwa kusema hivi: “Kwa kuchunguza maandishi yake, tunaona kwamba yamepungukiwa kihistoria. Hata sasa, visehemu vya Babyloniaca vina makosa mengi kuhusu mambo rahisi ya hakika . . . Mwanahistoria hapaswi kufanya makosa kama hayo, lakini kusudi la Berossus’ halikuwa kuandika habari za kihistoria.”3

      Kutokana na hayo, una maoni gani? Je, hesabu za Berossus zinapaswa kuonwa kuwa sahihi na zenye kutegemeka? Namna gani wanahistoria wengine wa kale, ambao mara nyingi, waliandika mfuatano wa matukio ya kihistoria wakitegemea maandishi ya Berossus? Je, kweli maelezo yao yanaweza kutegemeka?

  • Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya Kwanza
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
    • [Chati/​Picha katika ukurasa wa 29]

      (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

      WAFALME WA MILKI MPYA YA BABILONI

      Ikiwa wanahistoria hawa wanategemeka, kwa nini hawapatani?

      Wafalme

      Nabopolasa

      BEROSSUS m. 350-270 K.W.K.. (21)

      POLYHISTOR 105-? K.W.K. (20)

      JOSEPHUS 37-?100 W.K. (—)

      PTOLEMY m. 100-170 W.K. (21)

      Nebukadneza wa Pili

      BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (43)

      POLYHISTOR 105-? K.W.K. (43)

      JOSEPHUS 37-?100 W.K. (43)

      PTOLEMY m. 100-170 W.K. (43)

      Amel-Marduk

      BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (2)

      POLYHISTOR 105-? K.W.K. (12)

      JOSEPHUS 37-?100 W.K. (18)

      PTOLEMY m. 100-170 W.K. (2)

      Neriglissar

      BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (4)

      POLYHISTOR 105-? K.W.K. (4)

      JOSEPHUS 37-?100 W.K. (40)

      PTOLEMY m. 100-170 W.K. (4)

      Labashi-Marduk

      BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (miezi 9)

      POLYHISTOR 105-? K.W.K. (—)

      JOSEPHUS 37-?100 W.K. (miezi 9)

      PTOLEMY m. 100-170 W.K. (—)

      Nabonido

      BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (17)

      POLYHISTOR 105-? K.W.K. (17)

      JOSEPHUS 37-?100 W.K. (17)

      PTOLEMY m. 100-170 W.K. (17)

      (#) = Kipindi (cha miaka) ambacho wafalme walitawala kulingana na wanahistoria wa kale

      [Hisani]

      Photograph taken by courtesy of the British Museum

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki