-
Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa BabuloniUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
15. Kanisa Katoliki katika Ujeremani ya Nazi lilikuwaje na hatia ya damu katika visa viwili?
15 Katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany, Guenter Lewy anaandika: “Wakati Mashahidi wa Yehova walipokandamizwa katika Bavaria Aprili 13 [1933] Kanisa hata lilikubali mgawo liliopewa na Wizara ya Elimu na Dini wa kuripoti juu ya washiriki wa farakano hilo walioendelea kuzoea dini hiyo iliyokatazwa.” Hivyo Kanisa Katoliki linashiriki daraka la kupelekwa kwa maelfu ya Mashahidi kwenye kambi za mateso; mikono yalo imetiwa madoa ya damu ya uhai wa mamia ya Mashahidi ambao walinyongwa. Wakati Mashahidi vijana, kama Wilhelm Kusserow, walipoonyesha kwamba wangekufa kijasiri kwa kupigwa risasi na kikosi cha wapiga risasi, Hitla aliamua kwamba kikosi cha wapiga risasi hakikuwafaa wakataaji kidhamira; kwa hiyo Wolfgang ndugu ya Wilhelm, akiwa na umri wa miaka 20, alikufa kwa njia ya gilotini. Wakati ule ule, Kanisa Katoliki lilikuwa likiwatia moyo vijana Wakatoliki Wajeremani wafe katika jeshi la bara-baba lao. Hatia ya damu ya hilo kanisa yaonekana wazi!
-
-
Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa BabuloniUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 270]
Gharama ya Kuridhiana
Guenter Lewy anaandika katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany: “Kama Ukatoliki wa Ujeremani tangu mwanzo ungalishikamana na mwongozo wa kupinga kwa dhati utawala wa Nazi, historia ya ulimwengu ingaliweza kuchukua mwendo tofauti. Hata kama mng’ang’ano huu ungalikosa mwishowe kabisa kumshinda Hitla na kuzuia uhalifu wake mwingi, kwa oni hili ungaliinua sana hadhi ya kiadili ya Kanisa hilo. Gharama ya kibinadamu kwa ukinzani huu ingalikuwa kubwa bila kukanika, lakini dhabihu hizo zingalikuwa zimetolewa kwa ajili ya kusudi kubwa zaidi ya yote. Hitla akiwa haungwi mkono nyumbani, yamkini hangalithubutu kwenda vitani na kihalisi mamilioni ya maisha yangaliokolewa. . . . Wakati Wajeremani wapinga Unazi walipoteswa mpaka kifo katika kambi za mateso za Hitla, wakati weledi wa Polandi walipochinjwa, wakati mamia ya maelfu ya Warusi walipokufa kama tokeo la kutendwa kama Untermenschen [nusu-binadamu] wa Kislavi, na wakati binadamu 6,000,000 walipouawa kimakusudi kwa kuwa ‘si Waarya,’ maofisa wa Kanisa Katoliki katika Ujeremani walitegemeza utawala uliokuwa ukifanya uhalifu huu. Papa katika Roma, kichwa cha kiroho na mwalimu wa kiadili mkuu zaidi ya wote wa Kanisa Katoliki la Roma, alikaa kimya.”—Kurasa 320, 341.
-