-
Kujitahidi Kuwa WashindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
9. Mashahidi wa Yehova katika Ujeremani wa Nazi walitendwaje na Hitla, na kukiwa tendo-mwitikio gani kutoka viongozi wa kidini?
9 Wakati wa utawala wa Nazi katika Ujeremani, Hitla alipiga marufuku kabisa kabisa kazi ya kuhubiri ya Mashahidi wa Yehova. Kwa miaka kadhaa, maelfu ya Mashahidi walifungwa ndani ya kambi za mateso na magereza kikatili, ambako wengi walikufa, huku wanaume vijana 200 ambao walikataa kupigana katika jeshi la Hitla wakifishwa kwa amri ya serikali. Uungaji-mkono wa viongozi wa kidini wa yote haya unathibitishwa na maneno ya padri Mkatoliki, yaliyochapishwa katika ile nyusipepa The German Way ya Mei 29, 1938. Kwa sehemu, yeye alisema: “Sasa kuna nchi moja duniani ambako wale wanaoitwa eti . . . Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] wamekatazwa. Hiyo ni Ujeremani! . . . Wakati Adolf Hitla alipochukua mamlaka, nayo Episkopati ya Kikatoliki katika Ujeremani ikarudia ombi lao, Hitla akasema: ‘Hawa wanaoitwa eti Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] Wenye Bidii ni wafanyiza matata; . . . mimi nawaona kuwa wadanganyaji; mimi sivumilii kwamba Wakatoliki Wajeremani watatupiwa matope jinsi hiyo na huyu Mwamerika Jaji Rutherford. Mimi nafumua [Mashahidi wa Yehova] katika Ujeremani.’” Kwa hayo, yule padri akaongeza: “Hongera!”
-
-
Kujitahidi Kuwa WashindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Wakatoliki na Waprotestanti walisikia viongozi wao wa kidini wakiwahimiza washirikiane na Hitla. Ikiwa wao walipinga, wao walifanya hivyo kinyume cha maagizo kutoka kwa kanisa na serikali pia.”
-