Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Mambo ya Walawi
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Mei 15
    • IBADA TAKATIFU HUTAKA USAFI

      (Mambo ya Walawi 11:1–15:33)

      Masharti kuhusu wanyama safi na wasio safi yaliwanufaisha Waisraeli katika njia mbili. Yaliwakinga wasiambukizwe maradhi na vijidudu hatari, nayo yaliimarisha mpaka kati yao na mataifa yaliyowazunguka. Masharti mengine yalihusu uchafu uliotokana na mizoga, kutakaswa kwa wanawake baada ya kuzaa, hatua zilizopaswa kuchukuliwa kuhusiana na ukoma, na uchafu uliotokana na umajimaji unaotoka kwenye viungo vya uzazi vya wanaume na wanawake. Makuhani walipaswa kushughulikia watu ambao hawakuwa safi.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Mambo ya Walawi
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Mei 15
    • LAZIMA UTAKATIFU UDUMISHWE

      (Mambo ya Walawi 16:1–27:34)

      Dhabihu muhimu zaidi kwa ajili ya dhambi zilitolewa kila mwaka katika Siku ya Upatanisho. Ng’ombe-dume alitolewa kwa ajili ya makuhani na kabila la Lawi. Mbuzi alitolewa kwa ajili ya makabila ya Israeli ambayo hayakuwa makuhani. Mbuzi mwingine alipelekwa nyikani akiwa hai baada ya dhambi za watu kutangazwa juu yake. Mbuzi hao wawili walihesabiwa kuwa toleo moja la dhambi. Hayo yote yalionyesha kwamba Yesu Kristo angetolewa akiwa dhabihu na pia angechukua dhambi za watu.

      Masharti kuhusu kula nyama na kuhusu mambo mengine hukazia uhitaji wa kuwa watakatifu tunapomwabudu Yehova. Kwa kufaa, makuhani walipaswa kuendelea kuwa watakatifu. Sherehe tatu zilizofanywa kila mwaka zilikuwa pindi za kushangilia na kumshukuru Muumba. Yehova pia aliwapa watu masharti kuhusu kutumia vibaya jina lake takatifu, kushika Sabato na Yubile, na jinsi ya kuwatendea maskini na watumwa. Baraka ambazo zingetokana na kumtii Mungu zinatofautishwa na laana ambazo zingetokana na kutotii. Pia kuna masharti juu ya matoleo yaliyohusiana na nadhiri na makadirio, mzaliwa wa kwanza wa wanyama, na kutolewa kwa fungu la kumi kama ‘kitu kitakatifu kwa Yehova.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki