-
Urusi2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mnamo 1995 katika ofisi ya tawi ya Urusi, Dawati la Habari za Hospitali lilianza kufanya kazi ili kuwapa wataalamu wa kitiba habari sahihi kuhusu msimamo wa Mashahidi wa Yehova. Semina kadhaa zilifanywa, nao wazee kutoka zaidi ya Halmashauri 60 za Uhusiano na Hospitali walijifunza jinsi ya kuwapa madaktari na wataalamu wa kitiba habari zinazohitajika kutia ndani jinsi ya kuwapata madaktari ambao wangewatibu wagonjwa Mashahidi bila damu.
-
-
Urusi2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Madaktari wengi walibadili mtazamo kuhusu matumizi ya damu baada ya kufanya kazi na wawakilishi wa Dawati la Habari za Hospitali. Daktari mmoja wa upasuaji alisema hivi: “Nimeambiwa na wagonjwa [Mashahidi] na ninyi pia kwamba kukataa kwenu damu hakutegemei hisia bali kunategemea sheria ya Biblia. Niliamua kuthibitisha jambo hilo. Nilisoma mistari yote ya Biblia iliyonukuliwa katika habari mliyonipa. Baada ya kutafakari, nilikubali kwamba msimamo wenu unategemea Biblia. Lakini kwa nini makasisi hawasemi chochote kuhusu hilo? Sasa, mazungumzo kuhusu damu yanapotokea, ninawaambia madaktari wengine kuwa Mashahidi ndio wanaofuata Biblia.” Leo, zaidi ya madaktari 2,000 nchini Urusi huwatibu wagonjwa Mashahidi bila damu.
-