-
‘Umeumbwa kwa Njia ya Ajabu’!Amkeni!—2011 | Mei
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 3]
TUMEUMBWA TUSIPOTEZE NISHATI
Uwezo wetu wa kusimama na kutembea tukiwa wima unasaidia tusipoteze nishati kwa kuwa mtu hutumia misuli kidogo tu kusimama wima. Kwa kweli, ‘kiwango cha nishati tunachotumia kusimama kinazidi nishati tunayotumia kulala kwa asilimia 7 tu,’ anasema mtafiti wa mfumo wa neva John R. Skoyles. Anaongezea kusema kwamba mbwa anaposimama (kwa miguu minne) yeye hutumia asilimia 70 zaidi ya nishati kuliko ile anayotumia anapolala.
-
-
Thamini Uwezo Wako wa PekeeAmkeni!—2011 | Mei
-
-
Thamini Uwezo Wako wa Pekee
MWILI wa mwanadamu una uwezo mbalimbali wa pekee. Hakuna mnyama aliye na uwezo mbalimbali ambao wanadamu wanao. Sababu moja inayofanya tuwe na uwezo huo mbalimbali ni uwezo wetu wa kusimama wima, ambao zaidi ya kutusaidia kuona mbali, unatuwezesha kutumia mikono kufanya mambo mengine. Tungeshindwa kufanya mambo mengi sana iwapo tungetembea pia kwa mikono!
-