-
Kila Mtu Anahitaji MakaoAmkeni!—2005 | Septemba 22
-
-
Kila Mtu Anahitaji Makao
“Kila mtu ana haki ya kuishi chini ya hali zinazofaa kutia ndani . . . makao, kwa ajili ya afya na hali yake njema na ile ya familia yake.”—Azimio la Watu Wote la Haki za Binadamu, Kifungu cha 25.
-
-
Kila Mtu Anahitaji MakaoAmkeni!—2005 | Septemba 22
-
-
Haki ya Kila Mtu
Kila mwanadamu ana haki ya kuwa na nyumba inayofaa. Azimio la Watu Wote la Haki za Binadamu, lililopitishwa na Umoja wa Mataifa mwaka wa 1948, lilitangaza kwamba kila mtu ana haki ya kuishi chini ya hali zinazofaa, kutia ndani kuwa na makao yanayofaa. Kwa kweli, kila mtu anahitaji kuwa na nyumba nzuri.
Hivi karibuni, katika mwaka wa 1996, nchi kadhaa ziliidhinisha hati ya UM ambayo baadaye iliitwa Habitat Agenda. Hati hiyo inataja maazimio hususa ya kumwandalia kila mtu makao yanayofaa. Baadaye, katika Januari 1, 2002, UM liliimarisha azimio hilo kwa kufanya hati hiyo kuwa programu rasmi ya UM.
-