Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Hungaria

      Kila mara dada mmoja huletewa maziwa yakiwa kwenye chupa ndani ya mkoba ambao huning’inizwa kwenye ua wa nyumba yake. Siku moja, alipokuwa akirudisha chupa tupu, aliweka trakti Je, Ungependa Kujua Ukweli? kwenye ule mkoba. Kwa kushangaza, maziwa yalipoletwa tena, mwanamke ambaye husambaza maziwa hayo aliambatanisha karatasi iliyokuwa na maswali kuhusu trakti ile na ombi la kujifunza Biblia. Mara moja dada yetu alimtembelea mwanamke huyo kwenye shamba lake alikokuwa akiishi na kuanzisha funzo la Biblia kwa kutumia kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? Kabla ya hapo, mwanamke huyo alikuwa akitafuta majibu ya maswali hayo katika makanisa mbalimbali, lakini njaa yake ya kiroho haikuwa imetoshelezwa. Na katika harakati zake, badala ya kupata majibu, maswali yalikuwa yakiongezeka. Mmoja kati ya binti zake alipoanza kupendezwa pia, dada yetu alimpa kitabu Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu. Mama ya binti huyo alisema kwamba msichana huyo alikuwa akishtuka usiku kwa sababu ya kuota ndoto mbaya. Hata hivyo, baada ya kusoma baadhi ya sura katika kitabu hicho, binti yake hana woga naye hulala fofofo siku hizi. Mama huyo anaendelea kujifunza Biblia, naye anahudhuria mikutano ya Jumapili kwa ukawaida akiwa pamoja na binti zake wawili.

  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 60]

      Kuna njia nyingi za kuhubiri isivyo rasmi

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki