Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Silaha za Kibiolojia—Je, Kweli Ni Hatari?
    Amkeni!—2002 | Septemba 22
    • Kimeta: Ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria ya spora. Dalili za mapema za ugonjwa wa kimeta unaotokana na kuvuta hewa, zinafanana na zile za mafua. Baada ya siku kadhaa, mgonjwa hushindwa kupumua na hushikwa na mshtuko. Mara nyingi aina hiyo ya kimeta huua.

      Watu walio katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo wanaweza kujizuia kwa kutumia viuavijasumu. Ni muhimu mgonjwa atibiwe mapema; kuchelewa hupunguza uwezekano wa kupona.

      Si rahisi kuambukizwa ugonjwa wa kimeta kutoka kwa mtu mwingine, na huenda hata isitukie kamwe.

      Kuanzia mwaka wa 1950, ugonjwa wa kimeta ulianza kutumiwa kama silaha na nchi kadhaa, kutia ndani Marekani na ule uliokuwa Muungano wa Sovieti. Idadi ya mataifa yanayodhaniwa kuwa na silaha za kibiolojia yaliongezeka kutoka 10 mwaka wa 1989 hadi 17 katika 1995. Haijulikani ni mataifa mangapi kati ya hayo yanayotumia ugonjwa wa kimeta. Kulingana na uchunguzi mmoja uliofanywa na serikali ya Marekani, kunyunyiza kilogramu 100 za virusi vya kimeta katika jiji kubwa ni sawa na kurusha bomu la haidrojeni.

  • Silaha za Kibiolojia—Je, Kweli Ni Hatari?
    Amkeni!—2002 | Septemba 22
    • [Picha]

      Viini vya kimeta na spora ya mviringo

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki