Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Uwaheshimu Waliozeeka?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Mei 15
    • MTI mmoja ulio kando ya pwani ya California, huko Marekani ni kati ya miti inayopigwa picha nyingi zaidi duniani. Mti huo wa mvinje unaitwa Lone Cypress. Inaripotiwa kwamba mti huo umekuwapo kwa miaka zaidi ya 250. Mti huo wenye kuvutia sana unajulikana kwa sababu ya ustahimilivu wake na unatunzwa kwa njia mbalimbali. Kwa mfano, umeshikiliwa kwa nyaya na mawe yaliyowekwa kuzunguka shina lake.

      Mti huo unaweza kutukumbusha kuhusu Wakristo waliozeeka walio kati yetu ambao wanaonyesha uvumilivu mkubwa. Njia moja kuu ambayo wanafanya hivyo ni kwa kutangaza habari njema. Nabii Yoeli alitabiri kwamba “wazee” wangetangaza ujumbe wa Biblia. (Yoe. 2:28-32; Mdo. 2:16-21) Hebu fikiria saa nyingi ambazo waliozeeka wanatumia wakiwasaidia wengine kwa bidii kujifunza kuhusu “habari njema ya ufalme”! (Mt. 24:14) Wengine kati ya watangazaji hao wa Ufalme waliozeeka wamevumilia mateso au matatizo mengine kwa miaka mingi. Ikiwa mti tu wa mvinje unaheshimiwa kwa sababu ya kustahimili na unashikiliwa kwa mawe na nyaya, je, watu waliozeeka ambao wako kati yetu hawastahili kutegemezwa na kutendewa kwa heshima zaidi?

  • Kwa Nini Uwaheshimu Waliozeeka?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Mei 15
    • Bila shaka, washiriki wa familia wana daraka la pekee la kuwatunza wazazi, nyanya (bibi), na babu zao. Watu wametafuta njia za kuutunza mti wa Lone Cypress, na wanaendelea kufanya hivyo. Kwa hakika basi, tunapaswa kutafuta njia za kuendelea kuwaheshimu wazazi, nyanya, na babu zetu wanaozeeka. Kwa mfano, kuwa wasikilizaji wazuri kutatuzuia tusisisitize kufanya mambo kwa njia yetu bila kujali hisia zao.—Met. 23:22; 1 Tim. 5:4.

  • Kwa Nini Uwaheshimu Waliozeeka?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Mei 15
    • [Picha katika ukurasa wa 7]

      Kama vile mti wa “Lone Cypress” unavyohitaji kushikiliwa, waliozeeka wanahitaji kutendewa kwa heshima sana

      [Hisani]

      American Spirit Images/age fotostock

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki