Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mifano Inayofundisha
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
    • Yesu alisema wanafunzi wake ni “taa ya ulimwengu,” akafafanua kwa ufupi jinsi taa inavyotumiwa na jinsi usemi huo unavyohusiana na daraka lao. (Mt. 5:15, 16) Baada ya Yesu kutoa mfano wa kondoo aliyepotea, alitaja shangwe inayotokea mbinguni mtu mmoja mwenye dhambi akitubu. (Luka 15:7) Na baada ya Yesu kusimulia ile hadithi ya Msamaria mwenye ujirani, alimwuliza yule mtu swali hususa kisha akamshauri. (Luka 10:36, 37) Katika hali tofauti, Yesu aliwafafanulia watu wanyenyekevu waliotaka kujua mfano kuhusu aina mbalimbali za udongo na ule wa magugu shambani, lakini hakuufafanulia umati mifano hiyo. (Mt. 13:1-30, 36-43) Siku tatu kabla ya kufa, Yesu alitoa mfano unaohusu walimaji wa shamba la mizabibu waliokuwa wauaji. Hakueleza maana ya mfano huo kwa sababu hakukuwa na haja. “Makuhani wakuu na Mafarisayo . . . wakajua kwamba alikuwa akisema juu yao.” (Mt. 21:33-45) Kwa hiyo, mfano wako, maoni ya wasikilizaji, na kusudi lako ni muhimu katika kuamua iwapo utaeleza maana ya mfano huo na kadiri utakavyoufafanua.

  • Mifano ya Hali za Kawaida
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
    • Yesu Kristo alifanya nini? Yesu alipokuwa akizungumza na umati wa watu au na wanafunzi wake hakutumia mifano ya mambo ambayo hayakujulikana katika Israeli. Watu hawangeelewa mifano kama hiyo. Kwa mfano, Yesu hakutaja maisha katika makao ya kifalme kule Misri wala matendo ya kidini katika India. Lakini alitumia mifano ambayo ilihusu utendaji wa kawaida wa watu katika nchi zote. Alizungumzia kushona nguo, kufanya biashara, kupoteza kitu chenye thamani, na kuhudhuria sherehe za arusi. Alifahamu jinsi ambavyo watu hutenda katika hali mbalimbali, na alitumia vizuri hali hizo katika mifano. (Mk. 2:21; Luka 14:7-11; 15:8, 9; 19:15-23) Kwa kuwa Yesu alifundisha Waisraeli hasa, mara nyingi mifano yake iligusia vitu na utendaji uliokuwa kawaida katika maisha yao. Kwa hiyo, alitaja mambo kama ukulima, jinsi kondoo wanavyomtii mchungaji, na kuhifadhi divai katika ngozi za wanyama. (Mk. 2:22; 4:2-9; Yn. 10:1-5) Pia alitaja mifano ya matukio ambayo watu walielewa kama vile uumbaji wa wanadamu wawili wa kwanza, Furiko la siku za Noa, kuharibiwa kwa Sodoma na Gomora, kifo cha mke wa Loti, pamoja na mifano mingine. (Mt. 10:15; 19:4-6; 24:37-39; Luka 17:32) Unapochagua mifano ya kutumia, je, wewe pia hufikiria kwa makini mambo ambayo wasikilizaji hutenda kwa ukawaida na desturi zao?

      Namna gani kama unazungumza na mtu mmoja au labda watu wachache badala ya watu wengi? Jaribu kuchagua mfano ambao hasa unafaa vizuri watu hao wachache. Yesu alipomhubiria yule mwanamke Msamaria kwenye kisima kimoja karibu na Sikari, alitaja “maji yaliyo hai,” ‘kutopata kiu hata kidogo,’ na “bubujiko la maji linalobubujika ili kutoa uhai udumuo milele”—hizo zote ni semi zinazohusu utendaji wa mwanamke huyo. (Yn. 4:7-15) Na Yesu alipozungumza na wanaume waliokuwa wakiosha nyavu zao, alitumia semi zinazohusu uvuvi. (Luka 5:2-11) Katika hali hizo mbili, Yesu angalitaja mambo ya ukulima kwa sababu watu hao waliishi katika eneo la ukulima, lakini mifano yake ilikuwa na matokeo zaidi kwa sababu alitaja utendaji wao binafsi ili waelewe mambo wazi. Je, unajitahidi kufanya hivyo?

  • Mifano ya Hali za Kawaida
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
    • Yesu alitumia mambo rahisi ya kila siku badala ya kufanya ulinganifu unaotatanisha. Alitumia mambo madogo kufafanua mambo makubwa na mambo rahisi kufafanua mambo magumu. Yesu aliunganisha mambo ya kawaida na kweli za kiroho, akawasaidia watu kushika vizuri zaidi kweli hizo na kuzikumbuka. Huo ni mfano mzuri sana wa kuiga!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki