-
Kanuni UnazochaguaMnara wa Mlinzi—2002 | Februari 15
-
-
Kanuni huathiri maamuzi na mwendo tunaochukua maishani. Kanuni hutumika kama dira.
-
-
Kanuni UnazochaguaMnara wa Mlinzi—2002 | Februari 15
-
-
Mtazamo wa mimi kwanza unaweza kuwa kama sumaku. Na sumaku huathirije dira? Sumaku na dira zinapokaribiana, ncha ya dira huvutwa kuelekea sehemu tofauti. Katika njia hiyohiyo, mtazamo wa mimi kwanza, waweza kumvuruga mtu kwa kufanya kila kitu kionekane hakifai huku akishughulikia sana mambo ya ubinafsi na kuachilia mbali dira yake ya maadili au taratibu zake za mwenendo mzuri.
Je, ungeshangaa kujua kwamba mtazamo wa mimi kwanza haukuanza hivi karibuni? Mtazamo huo wa maisha ulianza katika bustani ya Edeni wakati wazazi wetu wa kwanza walipoacha viwango vya mwenendo mzuri ambavyo walipewa na Muumba wetu. Jambo hilo likapotosha dira yao ya maadili.
-