-
Hujui Ni Wapi Itafanikiwa!Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 15
-
-
a Maelezo yafuatayo ni marekebisho ya maelezo ya wakati uliopita katika gazeti la Mnara wa Mlinzi la Juni 15, 1992 (15/6/1992), ukurasa wa 17-22, na Mnara wa Mlinzi la Aprili 1, 1976, (1/4/1976) ukurasa wa 149-154 au toleo la Kiingereza la Oktoba 1, 1975 (1/10/1975), ukurasa wa 589-608, au la Kifaransa la Januari 15, 1976, (15/1/1976) ukurasa wa 45-50.
-
-
Hujui Ni Wapi Itafanikiwa!Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 15
-
-
4 Mfano huo unaonyesha ukuzi wa “ufalme wa Mungu,” kama inavyothibitishwa na kuenea kwa ujumbe wa Ufalme na kukua kwa kutaniko la Kikristo kuanzia Pentekoste ya mwaka wa 33 W.K. na kuendelea.
-
-
Hujui Ni Wapi Itafanikiwa!Mnara wa Mlinzi—2008 | Julai 15
-
-
6, 7. (a) Kumekuwa na ukuzi gani kuanzia mwaka wa 1914? (b) Kutakuwa na ukuzi gani mwingine?
6 Tangu Ufalme wa Mungu uliposimamishwa mbinguni mwaka wa 1914, matawi ya “mti” wa haradali yamepanuka kwa njia isiyotazamiwa. Watu wa Mungu wameona unabii huu wa Isaya ukitimizwa kihalisi: “Mdogo atakuwa elfu, na mnyonge atakuwa taifa lenye nguvu.” (Isa. 60:22) Kikundi kidogo cha watiwa-mafuta walioshiriki katika kazi ya kuhubiri kuhusu Ufalme mwanzoni mwa karne ya 20 hakingewazia hata kidogo kwamba kufikia mwaka wa 2008, Mashahidi wapatao milioni saba wangekuwa wakifanya kazi hiyo katika nchi zaidi ya 230. Kwa kweli, huo ni ukuzi mkubwa ajabu kama ukuzi wa mbegu ya haradali katika mfano wa Yesu!
7 Lakini je, ukuzi huo unakomea hapo? Hapana. Mwishowe raia wa Ufalme wa Mungu watajaa katika dunia yote. Wapinzani wote watakuwa wameondolewa. Jitihada za wanadamu hazitaleta mabadiliko hayo, bali Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova ndiye atakayeingilia kati na kuleta mabadiliko hayo duniani. (Soma Danieli 2:34, 35.) Ndipo tutakapoona utimizo wa mwisho wa unabii mwingine ulioandikwa na Isaya: “Dunia hakika itajawa na kumjua Yehova kama vile maji yanavyoifunika bahari.”—Isa. 11:9.
8. (a) Ndege walio katika mfano wa Yesu wanawakilisha nani? (b) Hata sasa tunalindwa kutokana na nini?
8 Yesu anasema kwamba ndege wa mbinguni wanapata makao chini ya kivuli cha Ufalme huo. Ndege hao hawawakilishi maadui wa Ufalme ambao wanajaribu kula mbegu nzuri, kama wale ndege wanaotajwa kwenye mfano wa mtu aliyetawanya mbegu katika udongo wa aina mbalimbali. (Marko 4:4) Badala yake, katika mfano huu ndege wanawakilisha watu wenye mioyo minyoofu ambao wanatafuta ulinzi ndani ya kutaniko la Kikristo. Hata sasa, watu hao wanalindwa kutokana na mazoea mapotovu na yenye kuchafua kiroho ya ulimwengu huu mwovu. (Linganisha na Isaya 32:1, 2.) Vivyo hivyo, Yehova aliulinganisha Ufalme wa Kimasihi na mti na kusema hivi kinabii: “Kwenye mlima wa kilele cha Israeli nitakipandikiza, nacho hakika kitazaa matawi na kutokeza matunda na kuwa mwerezi mkubwa. Na chini yake hakika watakaa ndege wote wenye mabawa ya kila aina; watakaa katika uvuli wa majani yake.”—Eze. 17:23.
-