Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Huwabariki na Kuwalinda Wale Wanaomtii
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • 1, 2. Kwa nini ni muhimu kumtii Mungu? Toa mfano.

      VIFARANGA wa rangi ya manjano wenye manyoya laini wanadonoa chakula katika nyasi fupi bila kujua kwamba kuna mwewe anayezunguka-zunguka juu. Kwa ghafula kuku atoa sauti ya juu yenye hofu na kukunjua mabawa yake. Vifaranga wanamkimbilia, na baada ya muda mfupi wote wako salama chini ya mabawa yake. Mwewe ashindwa kushambulia.a Tunajifunza nini? Kwamba utii huokoa uhai!

      2 Somo hilo ni muhimu hasa kwa Wakristo leo kwa kuwa Shetani anafanya kila awezalo ili awanase watu wa Mungu. (Ufunuo 12:9, 12, 17) Lengo lake ni kuharibu uhusiano wetu na Yehova ili tupoteze kibali chake na taraja la uhai udumuo milele. (1 Petro 5:8) Hata hivyo, tukimkaribia Mungu na kuitikia upesi mwelekezo tunaopokea kupitia Neno lake na tengenezo lake, tunaweza kuwa na uhakika kwamba Yehova anatulinda na anatujali. “Kwa manyoya yake atakufunika, chini ya mbawa zake utapata kimbilio,” akaandika mtunga-zaburi.—Zaburi 91:4.

      Taifa Lisilotii Lawa Windo

      3. Kwa sababu ya kutomtii Mungu mara nyingi, Waisraeli walipatwa na nini?

      3 Taifa la Israeli lilipomtii Yehova, aliendelea kuwatunza kwa uangalifu. Hata hivyo, mara nyingi watu hao walimwacha Mfanyi wao na kuabudu miungu ya miti na mawe—“vitu vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa.” (1 Samweli 12:21, 22) Baada ya uasi huo uliodumu kwa karne nyingi, taifa zima lilijihusisha sana na uasi-imani hivi kwamba halingeweza kurekebishwa. Kwa hiyo, Yesu aliomboleza hivi: “Yerusalemu, Yerusalemu, muuaji wa manabii na mpigaji kwa mawe wale waliotumwa kwake,—ni mara nyingi kadiri gani nilitaka kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku hukusanya vifaranga vyake pamoja chini ya mabawa yake! Lakini nyinyi watu hamkutaka hilo. Tazameni! Nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.”—Mathayo 23:37, 38.

  • Yehova Huwabariki na Kuwalinda Wale Wanaomtii
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • a Ingawa mara nyingi wanaonyeshwa kuwa waoga, “kuku watapigana hadi kifo kulinda vifaranga wao wasipatwe na madhara,” chasema kichapo kimoja cha shirika la kuwalinda wanyama.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki