-
Unaweza Kutumaini Uongozi wa Nani?Amkeni!—1996 | Novemba 8
-
-
“NI WAKATI wa kwenda!” baba amwambia mwana wake mwenye umri wa miaka mitano. Baba anyoosha mkono, na bila kusita mwana huyo anyoosha na kuviringisha mkono wake mdogo katika vidole vya baba yake. Bila kujali safari yaelekea wapi, mtoto huyo autumaini uongozi wa mzazi wake na aufuata akiwa na uhakika. Lolote litakalotokea, mtoto aendelea kushika kwa imara.
Kwa vile tunaishi katika siku zisizo na uhakika wa kiuchumi, kisiasa na kibinafsi, je, usingekaribisha mkono wenye kuongoza kutoka chanzo ambacho ungekitumaini kabisa? Lakini twaishi katika nyakati ambazo watu wasio wanyoofu hutumia vibaya watu wasio na uzoefu. Hivyo, kuna sababu ya kweli ya kuwa wenye tahadhari kwa mtu tumwaminiye. Katika nyakati za nyuma, labda ulitamaushwa kabisa ulipotegemea mtu fulani kwa uongozi lakini akakutamausha.
Hata hivyo, Biblia yatutia moyo kuweka tumaini letu katika Mungu. “Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope, mimi nitakusaidia,” alirekodi nabii Isaya. (Isaya 41:13) Na mtume Petro alishauri: “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”—1 Petro 5:6, 7.
-
-
Unaweza Kutumaini Uongozi wa Nani?Amkeni!—1996 | Novemba 8
-
-
Tena wacha turudie mfano wa mtoto anayeshika mkono wa mzazi wake. Mtoto awapo na wasiwasi, yeye hufanyaje? Badala ya kuacha au kupunguza mshiko wake, mtoto huyo atakaza mkono wake mdogo katika vidole vya mzazi wake. Kwa kufanya hivyo, aonyesha tumaini lake lisiloyumba-yumba kwamba mzazi huyo ataandaa uongozi usioshindwa na nguvu katika magumu.
Hali kadhalika, tupatapo mikazo katika maisha yetu, twapaswa kukaza mshiko wetu, tukitumaini hata zaidi katika uongozi wa Mungu! Neno lake, Biblia, laweza kuwa nuru ya kutuongoza. (Zaburi 119:105) Pia, kumbuka kwamba pamoja na tumaini huja subira. Kwa sababu hiyo, twapaswa kumpa Yehova wakati ili asuluhishe matatizo, hata ikiwa kwa kipindi fulani cha wakati hatuwezi kuelewa sana kwa nini anatuongoza katika njia fulani. Naam, twaweza kutumaini uongozi wa Mungu.—Kutoka 15:2, 6; Kumbukumbu la Torati 13:4; Isaya 41:13.
-