-
Unaweza Kudumisha Usafi wa Kiadili Katika Ulimwengu Usio na MaadiliMnara wa Mlinzi—2000 | Julai 15
-
-
Matokeo ya ukosefu wa adili kingono ni machungu kama pakanga na makali kama upanga wenye makali kuwili, yaani ni machungu na huleta kifo. Dhamiri mbaya, mimba haramu, au maradhi yenye kuambukizwa kingono kwa kawaida ndiyo matokeo machungu ya mwenendo wa aina hiyo. Na ebu fikiria maumivu makali ya kihisia-moyo yanayompata mwenzi wa ndoa wa mtu asiye mwaminifu. Tendo moja la uzinzi laweza kuleta maumivu yenye kudumu maishani. Naam, ukosefu wa adili huumiza.
-
-
Unaweza Kudumisha Usafi wa Kiadili Katika Ulimwengu Usio na MaadiliMnara wa Mlinzi—2000 | Julai 15
-
-
Hasara Kubwa Mno
Tuna sababu gani nyingine ya kujitenga mbali na njia za mtu mpotovu? Solomoni anajibu: “Usije ukawapa wengine heshima yako, na wakorofi miaka yako; wageni wasije wakashiba nguvu zako; kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, nyama yako na mwili wako utakapoangamia.”— Mithali 5:9-11.
Hivyo Solomoni anakazia ile hasara kubwa ya kushindwa na ukosefu wa adili. Uzinzi na kujipotezea heshima huambatana pamoja. Je, kwa kweli si jambo la kujifedhehesha kutumika tu kama chombo cha kutosheleza harara zako au za mtu mwingine zisizo za adili? Na si kukosa kujistahi unapojiingiza katika mahusiano ya kingono na mtu ambaye si mwenzi wako wa ndoa?
Lakini ‘kuwapa wakorofi au wageni miaka yetu, nguvu zetu, na kazi zetu’ hutia ndani nini? Kitabu kimoja cha marejezo chataarifu hivi: “Jambo kuu katika mistari hii liko wazi kabisa: Uzinzi huenda ukaleta hasara kubwa; kwa kuwa kila kitu ambacho mtu hujitaabisha kutafuta—wadhifa, uwezo, ufanisi—vyote hivyo vyaweza kupotea kutokana na madai yenye pupa ya mwanamke huyo au malipo ya kufunika aibu ya ukoo wa watu wake.” Ukosefu wa adili kingono waweza kuleta hasara kubwa!
Baada ya kupoteza heshima na mali yake, mtu mpumbavu huguna, akisema: “Jinsi nilivyochukia maonyo, na moyo wangu ukadharau kukemewa; wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, katikati ya mkutano na kusanyiko.”— Mithali 5:12-14.
Hatimaye, mwenye dhambi huyo husema maneno ambayo msomi mmoja ayaita “orodha ndefu ya ‘laiti ninge . . . ’: laiti ningemsikiliza baba yangu; laiti ningeacha kujitegemea mwenyewe; laiti ningesikiliza mashauri ya wengine.” Hata hivyo, utambuzi huo huja ukiwa umechelewa mno. Kufikia hapo maisha machafu na adhama ya mtu huyo huwa yameharibika kabisa. Jinsi ilivyo muhimu sana kwetu kufikiria kwa uzito hasara kubwa ya kushiriki katika ukosefu wa adili kingono kabla ya kumezwa ndani yake!
-