-
Tumaini Zuri Zaidi kwa Ajili ya NafsiMnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 1
-
-
Wayahudi hawakupata wazo hili kutoka katika Biblia, bali kutoka kwa Wagiriki. Yaonekana hiyo dhana ilitoka katika madhehebu ya kidini yenye mafumbo ya Kigiriki na kuingia falsafa ya Kigiriki, kati ya karne ya saba na tano K.W.K. Wazo la kuwako kwa uhai baada ya kifo ambako nafsi mbaya zingepokea malipo yenye maumivu lilikuwa limewavutia watu wengi kwa muda mrefu, na hiyo dhana ikaimarika na kuenea. Wanafalsafa walibishana daima juu ya hali hususa ya nafsi. Homer alidai kwamba nafsi ilihama upesi wakati wa kifo, ikifanya sauti yenye kusikika ya kuvuma, mlio mwembamba mkali, au ya mchakacho. Epicurus alisema kwamba kwa kweli nafsi ilikuwa na uzani na basi ilikuwa na mwili mdogo mno.d
Lakini yule ambaye labda ndiye mwenye kuunga mkono zaidi kutokufa kwa nafsi alikuwa Plato, mwanafalsafa Mgiriki wa karne ya nne K.W.K. Ufafanuzi wake wa kifo cha mwalimu wake, Socrates, wafunua masadikisho yaliyofanana sana na yale ya Wazeloti wa Masada karne kadhaa baadaye. Kama vile msomi Oscar Cullmann aelezavyo, “Plato atuonyesha jinsi Socrates anavyokufa katika hali ya amani na utulivu kamili. Kifo cha Socrates ni kifo kizuri sana. Tisho la kifo halionekani hata kidogo. Socrates hawezi kuhofu kifo, kwa maana hicho kwa kweli hutuweka huru na mwili. . . . Kifo ni rafiki mkubwa wa nafsi. Ndivyo [Socrates] afundishavyo; na ndivyo anavyokufa, kwa kupatana vizuri ajabu na fundisho lake.”
-
-
Tumaini Zuri Zaidi kwa Ajili ya NafsiMnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 1
-
-
Basi, ni kwa nini twaona makanisa ya Jumuiya ya Wakristo yakifundisha kutokufa kwa nafsi ya kibinadamu badala ya ufufuo? Fikiria hili jibu lililoandaliwa na mwanatheolojia Werner Jaeger katika The Harvard Theological Review huko nyuma katika 1959: “Jambo la hakika la maana zaidi katika historia ya mafundisho ya Kikristo lilikuwa kwamba yule baba wa theolojia ya Kikristo, Origen, alikuwa mwanafalsafa wa Kiplato kwenye shule ya Alexandria. Aliongezea mafundisho ya Kikristo yale mafundisho mengi kuhusu kutokufa kwa nafsi, aliyotwaa kutoka kwa Plato.” Kwa hiyo kanisa lilifanya sawa tu na vile Wayahudi walivyokuwa wamefanya karne kadhaa mapema! Yalipuuza mafundisho ya Kibiblia kwa kupendelea falsafa ya Kigiriki.
-