Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Vito vya Kingo za Mto
    Amkeni!—1997 | Juni 22
    • Kereng’ende wana mabawa mawili yenye kupindika na yaliyo mepesi. Ingawa mabawa hayo huonekana kuwa dhaifu, hayo yaweza kupiga mara 40 kwa sekunde moja nayo huweza kustahimili kugongwagongwa bila kupatwa na madhara. Mwanabiolojia Robin J. Wootton ayafafanua kuwa “maajabu madogo ya ubuni wenye ustadi.”

      “Kadiri tuelewavyo zaidi kazi ya mabawa ya mdudu,” yeye aongezea, “ndivyo ubuni wayo na umaridadi wa uumbaji wayo uzidivyo kuonekana. . . . Mabawa ya wadudu hayana kifani katika tekinolojia.” Haishangazi kwamba mbinu za mruko wa kereng’ende zinachunguzwa sasa na wahandisi wa ndege.

  • Vito vya Kingo za Mto
    Amkeni!—1997 | Juni 22
    • Wanasayansi wengi wa mageuzi humfikiria kereng’ende kuwa mdudu wa kuruka wa mapema zaidi kati ya wadudu. Kisukuku kimoja kilichovumbuliwa nchini Ufaransa kilitokeza kwenye miamba kereng’ende fulani mwenye mabawa yenye upana wa sentimeta 75! Ndiye mdudu mkubwa zaidi ajulikanaye, akiwa mkubwa zaidi ya mara tatu kuliko kereng’ende yeyote aishiye.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki