Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Usingizi Ni Starehe Tu au Ni Muhimu?
    Amkeni!—2003 | Machi 22
    • Inaonekana usingizi huathiri pia hamu yetu ya kula. Wanasayansi wamegundua kwamba kwa kweli usingizi ni “njia kuu ya asili inayoburudisha” kama alivyosema Shakespeare. Ubongo wetu huona ukosefu wa usingizi kuwa ukosefu wa chakula. Tunapolala, mwili wetu hutengeneza homoni inayoitwa leptin, inayojulisha mwili wetu kwamba tumeshiba. Tunapokuwa macho kwa muda mrefu sana, mwili wetu hutengeneza kiasi kidogo cha leptin, na kutufanya tutamani sana chakula cha wanga. Kwa hiyo, kukosa usingizi kunaweza kutufanya tule chakula kingi cha wanga, na hivyo tunenepe kupita kiasi.

  • Usingizi Ni Starehe Tu au Ni Muhimu?
    Amkeni!—2003 | Machi 22
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 6]

      MATOKEO YA KUKOSA USINGIZI

      MATOKEO YA MUDA MFUPI

      ◼ Kusinzia

      ◼ Hisia zinazobadilika- badilika

      ◼ Kusahau mambo kwa muda mfupi

      ◼ Kushindwa kupanga mambo na kuyatimiza

      ◼ Kutokuwa makini

      MATOKEO YA MUDA MREFU

      ◼ Kunenepa kupita kiasi

      ◼ Kuzeeka mapema

      ◼ Uchovu

      ◼ Hatari kubwa ya kupatwa na maambukizo, ugonjwa wa sukari, magonjwa ya moyo, na matatizo ya tumbo

      ◼ Kusahau mambo sana

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki