-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Wamoabi watalia kwa sababu ya mikate ya zabibu ya Kir-haresethi, ambayo labda ni zao kuu la jiji hilo. (Isaya 16:6, 7) Sibma na Yazeri, miji maarufu kwa ukuzaji wa zabibu, itapigwa. (Isaya 16:8-10)
-
-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Isaya mwenyewe, akiwa na uhakika kuhusu kutimizwa kwa hukumu hizo, apata hisia kali. Sawa na kamba za kinubi zenye kutikisika, sehemu zake za ndani zakumbwa na sikitiko kwa sababu ya ujumbe wa ole dhidi ya Moabu.—Isaya 16:11, 12.
12. Maneno ya Isaya dhidi ya Moabu yalitimizwaje?
12 Unabii huo utatimizwa lini? Hivi karibuni. “Hilo ndilo neno lile alilolisema BWANA juu ya Moabu zamani. Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, pamoja na wingi wake wote; mabaki yake yatakuwa machache sana, kama si kitu kabisa.” (Isaya 16:13, 14) Kwa kupatana na hayo, kuna uthibitisho wa kiakiolojia kwamba, mnamo karne ya nane K.W.K., Moabu iliteseka sana na sehemu nyingi nchini mwake zikaachwa ukiwa. Tiglath-pilesa wa Tatu alimtaja Salamanu wa Moabu miongoni mwa watawala waliomlipa ushuru. Senakeribu alipokea ushuru kutoka kwa Kamusunadbi, mfalme wa Moabu. Watawala wa Ashuru, Esar-hadoni na Ashurbanipali walisema kuwa waliwatawala Wafalme Musuri na Kamashaltu wa Moabu. Karne kadhaa zilizopita, Wamoabi walikoma kuwa kikundi cha watu. Magofu ya majiji yanayodhaniwa kuwa ya Wamoabi yamevumbuliwa, ingawa hadi sasa kuna uthibitisho mchache ambao umefukuliwa unaohusu adui huyo wa Israeli ambaye hapo awali alikuwa mwenye nguvu sana.
-
-
Shauri la Yehova Dhidi ya MataifaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Hata hivyo, kuna tumaini kwa watu katika “Moabu” ya siku ya kisasa. Katikati ya unabii wake dhidi ya Moabu, Isaya asema: “Kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.” (Isaya 16:5) Mwaka wa 1914, Yehova alikisimamisha imara kiti cha ufalme cha Yesu, Mtawala katika ukoo wa Mfalme Daudi. Umaliki wa Yesu ni wonyesho wa rehema ya Yehova, nao utadumu milele, kwa kutimiza agano la Mungu pamoja na Mfalme Daudi. (Zaburi 72:2; 85:10, 11; 89:3, 4; Luka 1:32) Wasikivu wengi wameacha “Moabu” ya siku ya kisasa nao wamejitiisha chini ya Yesu ili wapate uhai. (Ufunuo 18:4) Inawafariji kama nini kujua kwamba Yesu ‘atafanya lililo haki kuwa wazi kwa mataifa’!—Mathayo 12:18; Yeremia 33:15.
-