Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wahama-Hamaji wa Asia Waliofanyiza Milki
    Amkeni!—2008 | Mei
    • Baada ya kudhibiti njia za biashara kati ya China na Bahari ya Mediterania kuelekea pande za mbali za magharibi, Genghis Khan alijaribu kufanya mapatano ya kibiashara pamoja na Sultani Muhammad wa Uturuki. Sultani huyo alitawala milki kubwa katika eneo ambalo leo linatia ndani Afghanistan, Tajikistan, Turkmenistan, Uzibekistani, na sehemu kubwa ya Iran.

      Katika 1218 wajumbe Wamongol, ambao inaelekea walitaka kufanya biashara, walifika katika mpaka wa eneo la sultani huyo. Lakini gavana wa eneo hilo aliwaua, na hivyo akaanzisha matukio ambayo yaliwafanya Wamongol wavamie kwa mara ya kwanza nchi ya Kiislamu. Katika miaka mitatu iliyofuata, Wamongol, waliosemekana kuwa wengi kuliko chungu, walipora, wakateketeza majiji na mashamba, na kuwaua raia wengi wa Sultani Muhammad, isipokuwa wale waliokuwa na ustadi ambao Wamongol walitaka.

      Kisha, jeshi la Mongol lililokadiriwa kuwa na askari 20,000 hivi likapita maeneo ya Azerbaijan na Georgia kuelekea nchi tambarare iliyo kaskazini ya Caucasia likishinda majeshi yote waliyokutana nayo, kutia ndani jeshi la Urusi lenye askari 80,000. Katika safari ya kilomita 13,000 hivi, Wamongol walizunguka Bahari ya Kaspiani katika kile kinachoonwa na watu fulani kuwa mojawapo ya uvamizi mkubwa zaidi wa jeshi la wapanda-farasi katika historia. Mfululizo wao wa ushindi uliweka kielelezo cha uvamizi ambao ungefuata wa Ulaya Mashariki na watawala wa baadaye wa Mongol.

  • Wahama-Hamaji wa Asia Waliofanyiza Milki
    Amkeni!—2008 | Mei
    • Mashambulio Mengine Katika Maeneo Mawili

      Khan Mkuu aliyefuata alikuwa Mongke, ambaye alitawazwa mnamo 1251. Yeye na nduguye Kublai walishambulia milki ya Sung kusini mwa China, huku jeshi lingine likishambulia maeneo ya magharibi. Jeshi lililoelekea magharibi liliharibu Baghdad na likalazimisha Damasko lisalimu amri. Watu waliodai kuwa Wakristo waliokuwa wakipambana na Waislamu walifurahi sana, na “Wakristo” walioishi Baghdad walipora na kuwaua majirani wao Waislamu.

      Wakati huo muhimu sana—Wamongol walipokuwa tu tayari kumaliza jamii ya Waislamu—historia ilijirudia. Walipata ujumbe kwamba Mongke amekufa. Kwa mara nyingine tena, wavamizi hao walirudi nyumbani, wakati huu wakiwaacha wanaume 10,000 waulinde mpaka. Muda mfupi baada ya hapo, jeshi hilo lenye watu wachache liliangamizwa na jeshi la Wamisri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki