Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Muumba Ajifunua—Kwa Manufaa Yetu!
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • Hilo lilitukia kwa sababu Farao alibadili maoni yake upesi. Aliongoza jeshi lake kuwakimbiza kwa bidii wale watumwa waliokuwa wakienda, akiwafikia karibu na Bahari Nyekundu. Waisraeli walinaswa kati ya bahari na jeshi la Misri. Kisha Yehova akaingilia kwa kufungua njia kupitia Bahari Nyekundu. Farao angalipaswa kutambua kwamba huo ulikuwa wonyesho wa uwezo wa Mungu usioweza kushindwa. Badala yake, yeye aliongoza jeshi lake himahima kufuata Waisraeli—akazama na jeshi lake Mungu aliporudisha bahari katika hali yake ya kawaida. Masimulizi yaliyo katika Kutoka hayasemi kihususa jinsi Mungu alivyotimiza matendo hayo. Twaweza kuyaita kwa haki kuwa miujiza kwa sababu matendo hayo na wakati yalipotukia hayangeweza kuongozwa na wanadamu. Kwa hakika, matendo kama hayo hayangemshinda Yule aliyeuumba ulimwengu pamoja na sheria zake zote.—Kutoka 14:1-31.

  • Muumba Ajifunua—Kwa Manufaa Yetu!
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
    • Kwa mfano, gazeti New Scientist liliripoti kwamba wataalamu wawili wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Tokyo walitumia sumaku yenye nguvu sana kwenye mrija uliolazwa ambao ulitiwa maji kwa kiasi. Maji yalikimbilia miisho ya huo mrija, sehemu ya katikati ikakauka. Tukio hilo, lililogunduliwa mnamo 1994, linatokea kwa sababu maji husukumwa kihafifu na sumaku. Tukio hilo lililothibitishwa la maji kutoka penye nguvu nyingi za sumaku hadi mahali ambapo hapana nguvu nyingi za sumaku limeitwa Athari ya Moses. Gazeti New Scientist lilisema kwamba: “Ni rahisi kusukuma-sukuma maji—ikiwa una sumaku kubwa ya kutosha. Na ikiwa hivyo, karibu kitu chochote kinawezekana.”

      Bila shaka, mtu hawezi kusema kwa uhakika kabisa njia ambayo Mungu alitumia kugawanya Bahari Nyekundu kwa ajili ya Waisraeli. Lakini, Muumba ajua kabisa sheria zote za asili. Yeye angeweza kudhibiti kwa urahisi sehemu fulani ya sheria moja kwa kutumia sheria nyinginezo ambazo alifanyiza. Kwa wanadamu, matokeo yaweza kuonekana kuwa ya kimuujiza, hasa kama hawakujua vizuri sheria zilizohusika.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki