-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha Samweli wa KwanzaMnara wa Mlinzi—2005 | Machi 15
-
-
NI MWAKA wa 1117 K.W.K. Miaka 300 hivi imepita tangu Yoshua akamilishe ushindi wa Nchi ya Ahadi. Wanaume wazee wa Israeli wanamjia nabii wa Yehova wakiwa na ombi lisilo la kawaida. Nabii huyo anasali kuhusu jambo hilo, naye Yehova anakubali ombi lao. Hilo linaonyesha wazi mwisho wa kipindi cha Waamuzi na mwanzo wa enzi ya wafalme wa kibinadamu. Kitabu cha Biblia cha Samweli wa Kwanza kinaeleza matukio yenye kusisimua yanayotukia katika kipindi hicho muhimu cha badiliko katika historia ya taifa la Israeli.
-
-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha Samweli wa KwanzaMnara wa Mlinzi—2005 | Machi 15
-
-
MFALME WA KWANZA WA ISRAELI —JE, ALIFANIKIWA AU HAKUFANIKIWA?
Samweli ni mwaminifu kwa Yehova maisha yake yote, lakini wanawe hawatembei katika njia za Mungu. Wanaume wa Israeli wanapoomba mfalme wa kibinadamu, Yehova anakubali ombi lao. Samweli anafuata mwongozo wa Yehova naye anamtia mafuta Sauli, Mbenyamini mwenye sura nzuri, awe mfalme. Sauli anaimarisha cheo chake akiwa mfalme kwa kuwashinda Waamoni.
-